
China imeipiga marufuku Marekani kutumia anga lake kufanya uchunguzi wa
silaha za nyuklia dhidi ya Korea Kaskazini mara baada ya kuidhibiti
ndege ya kufanya uchunguzi kutoka Marekani liliyokuwa inatumia anga la
nchi hiyo.
Aidha, ndege hiyo ilitumwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi dhidi ya
mionzi ya silaha za nyuklia yaliyofanywa na Korea Kaskazini ambapo baada
ya ndege hiyo kuingia anga la China ilishushwa mara moja na ndege za
kijeshi za China.
Ikizungumzia hatua hiyo iliyochukuliwa na China, Marekani imesema kuwa
China imetumia nguvu kubwa kuishusha ndege hiyo kwani ilikuwa katika
doria ya kwaida katika shughuli za kijeshi za anga.
Hata hivyo, China imeonya hatua hiyo ya Marekani kuwa inaweza
kuhatarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo. kwani
kuingilia anga la nchi hiyo bila taarifa ni kufanya makosa