Katika mazungumzo yao, Mhe
MAKONDA na Bi. COOKE wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya
majiji makubwa mawili Dar es salaam Tanzania na London nchini
Uingereza, makubaliano ambayo yatasaidia kupatikana kwa vifaa vya kisasa
vya kuzuia na kupambana na majanga kama vile moto na mafuriko, ambapo
Mhe MAKONDA ameomba kupatiwa magari ya kisasa ya shughuli za kuzima moto
na uokoaji.
Mhe MAKONDA pia ameomba kusaidiwa
vifaa maalum vya UTAMBUZ*I wa mifumo ya teknolojia ya kamera za kisasa
zitakazofungwa *barabarani kwa ajili ya kusaidia USALAMA wa magari, raia
na mali zao mifumo ambayo inafanya kazi katika jiji la London nchini
Uingereza, hatua itakayokwenda sambamba na ujengewaji UWEZO kwa maofisa
wa polisi wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya mifumo hii.
Katika kukabiliana na changamoto
ya MIGOGORO ya ARDHI mkoani Dar es salaam, Mhe MAKONDA ameomba kusaidiwa
kuwajengea uwezo maafisa ARDHI na Mipango miji wa Mkoa wa Dar es salaam
katika matumizi ya kisasa ya upimaji na upangaji ardhi, mafunzo ambayo
yatakwenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kupima ardhi,
jambo litakalosaidia kuondoa KERO ya upatikanaji wa HATI pamoja na
vibali vya UJENZI Mkoa wa Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo, Mhe
MAKONDA na Bi. COOKE wamejadili suala la uanzishwaji wa JIJI la FIKRA
(brain storming center ) kwa ajili ya kuwakutanisha vijana wabunifu kama
ilivyo kwa Tech City Uingereza.
Katika kuhitimisha mazungumzo
yao, Mhe MAKONDA na Bi. COOKE kwa pamoja wamekubaliana kuzikutanisha
timu za wataalamu kutoka London na Dar es salaam za kukabiliana na
Majanga haraka iwezekanovyo.
Bi. COOKE, kwa upande wake
amefurahishwa na jinsi Mkuu wa Mkoa anavyopambana na vita ya dawa za
kulevya ambayo imeathiri nguvu kazi kubwa sana katika jiji la Dar es
salaam na kumuhakikishia kuwa Serikali ya Uingereza inaunga mkono
jitihada zote zinazofanywa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa
wa Dar es salaam.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
23/05/2017.
23/05/2017.