
Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ametoa pole kwa familia
zilizopatwa na msiba kufuatia ajali iliyotokea jana Jijini Arusha na
kusababisha vifo zaidi ya 30.
Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kwa niaba ya
wananchi wa jimbo la Nzega amewatia moyo wanafamilia wote na Taifa kwa
ujumla kufuatia msiba huu na kuwataka watanzania wote kuwa tayari kwa
safari hii.
"Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nzega niwape pole familia za watoto
hawa waulim na madereva ambao mwenyezi Mungu amewaita mbele ya haki" -
Hussein Bashe.
"Kila nafsi itaonja mauti na mwenyezi Mungu amewaita hawa binadaam
wenzetu katika umri mdogo wakati wazazi wao, familia zao na Taifa likiwa
na matarajio makubwa na matumaini makubwa, ila Allah hutupima imani
zetu kwa majaribu makubwa kama haya, tumshukuru kwa kila jambo na sisi
tujiandae kwa safari hii ya asili na kimaumbile" - aliongeza Bashe.
"Poleni wanafamilia, poleni walimu, poleni watanzania wote"- Hussein Bashe.
Tags
Bashe