
Kumekuwepo na uvumi kuwa eti Tanzania imenunua ndege mbovu aina ya
boeing 787-8 Dreamliner ambayo ni Terrible Teen line number 19 yenye
serial number 35508.
Uvumi huo na uchochezi huo ulienezwa na kukolezwa zaidi na mbunge wa
Kigoma mjini mh. ZK kwenye mitandao yake ya kijamii zikiwemo akaunti
zake za facebook na twitter kuwa eti serikali imenunua ndege TT
liyokatataliwa na Rwanda na Moroko yenye line #19 kwa bei ya ndege mpya
na ZK kupata uungwaji mkono wa watanzania wengi.
Mh. ZK amekuwa akitoa ushahidi kutoka vyanzo visivyo na uhakika kama
b787register.com, chanzo ambacho kimeweka taarifa kuwa ndege hiyo
itakuwa delivered kwa Air Tanzania mwezi Agosti 2017 kitu ambacho ni
uongo.
Ikumbukwe kuwa baada ya mazungumzo kati ya Rais wa Tanzania na
Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya ndege ya Boeing Bw. Jim
Deboo, Rais wa Tanzania alisema kuwa ndege inayonunuliwa na Tanzania
itawasili mwezi juni mwaka 2018.
Katika majibu yake bungeni kwa swali lililoulizwa na mh.ZZK , waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa alikanusha uvumi kuwa
Tanzania imenunua ndege ambayo ni Terrible Teen yenye line#19 na
kubainisha wazi kuwa taarifa hizo ni za uongo na ukweli ni kwamba ndege
ya boeing 787-8 iliyonunuliwa na Tanzania ni mpya kabisa na ina line
#719 .
Sijui kwa kutafuta kick zaidi, mh ZK akazidi kutweet kuwa eti Mh Waziri
amedanganya bunge anaficha ukweli na hata mh mbunge huyo kutweet
akiwauliza Boeing kuhusu TT line #19 kuuzwa kwa Tanzania kwa bei ya
mpya, uzuri Boeing hawakumjibu.
Sasa imekuja kudhihirika kuwa maneno ya Waziri ni sahihi kuwa Tanzania
imenunua ndege mpya ya Boeing 787-8 yenye line #719. Ndege 787-8 TT
yenye line #19 imechukuliwa na kampuni nyingine
Woodys AeroImages na 787blogger kupitia akaunti zao za twitter
wamethibitisha kuwa ndegeiliyonunuliwa na Tanzania kutoka Boeing ni
yenye line #719
My Take: Nawashauri wanasiasa wasiingize siasa katika mambo ya msingi ya
maendeleo ya Taifa kwa ajili ya manufaa yao kisiasa, hiyo inaweza
kuwaharibia na wakati mwingine kupoteza imani kwa wananchi
Tags
ndege mpya
