
Kwa mujibu wa dini ya kiislam tunakumbushwa kuwa kila muislam mzima na
mwenye afya njema anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya
kufunga chakula na kinywaji mcahana na kutwa sambamba na kujizuia
kushiriki toka alfajiri hadi magharibi.
Pamoja na hayo, matendo hayo yatoba hupaswa kuendana na kuswali sana pamoja na kusoma quran kwa wingi.
Katika mwezi huu wa Ramadhani kadhalika inatakiwa kwa muislam kuwa mengi
ya maneno yake yawe katika kumtaja Allah (Subhaanahu wa Ta’ala), kwani
ni jambo ambalo linasaidia katika kuusafisha moyo wake na kuiboresha
funga yake.
Mbali na hayo zipo pia faida nyingine za kufunga kama zifuatazo
1. Ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na
faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho.
2. Faida ya pili ya mfungaji wa swaumu ni kujizoesha kuwa na subira,
yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mtu anajifunza jinsi ya kuwa
mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili.
3. Faida nyingine ni kuwa muadilifu na kujifundisha usawa baina ya masikini na tajiri.