
Utoaji wa mimba limekuwa jambo sugu na linalokuwa kwa kasi sana hasa kwa
wasichana bila kufahamu madhara yake.sababu kuu ya kutoa mimba ni
kupata ujauzito bila kuwa na mpango maalumu na mwenza wake,
wasichana wengi Hubeba mimba shuleni. jambo lakushangaza Imekuwa la
kawaida sana kwa watu walio kwenye mahusiano, kwani wamekuwa wakipuuzia
matumizi ya kinga kwa kujidanganya utamu wa mapenzi kupungua,wakati
huohuo wakijua kuna madhara mengi sana kufanya Tendo hilo bila
kuzingazitia matokeo baada ya uzembe huo…
Madhara yanayoambatana na utoaji mimba ni
vifo, kupoteza damu nyingi, kifafa cha uzazi na maambukizi hatarishi katika mfuko wa uzazi au mirija ya uzazi.
Haya yote yanaambatana na homa kali na maumivu makali, kutunga usaha
kwenye kizazi na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa dharura au haraka
kitaalamu; kikubwa mara nyingi ni kifo.
Mhusika kama akipona kutokana na athari ya kuichokonoa mimba visivyo au kwa nguvu sana,
wakati mwingine husababisha uharibifu wa mfuko wa uzazi na mirija yake,
na hubakiwa na makovu kwenye ile ngozi laini ya mfuko wa uzazi, ambayo
humsababishia maumivu makali anapokaribia siku zake za hedhi ama
kuupoteza mzunguuko wake. Hii ni kwa muda mrefu au milele. Kitaalamu
wanaita ni kupoteza heshima ya uzazi (quality of life).
Athari nyingine ni kufungwa kwa kizazi, kwamba mirija ya uzazi ikijifunga basi mwanamke huyo hawezi tena kuzaa maishani mwake.
Kutokana na kujifunga kwa mirija ya uzazi, athari ni kuwa mbegu ya yai
la mwanaume ambayo ni ndogo hujipenyeza na kuingia, na mbegu ya yai la
mwanamke ambayo ni kubwa hupita na yanapokutana kusabibisha mimba
kutunga nje ya kizazi, ambayo kitaalamu huitwa “ectopic pregnancy”.
Kwa kuwa mimba hiyo iko nje ya mazingira ya kawaida, inaweza ikapasuka
na kupoteza damu nyingi na kusababisha kifo na ikiwahiwa ni kufanyiwa
upasuaji na kulifunga eneo hilo.
Athari nyingine ni ugumba ambao kitaalamu unajulikana kama
“infertility”. Hali hii inatokana na uharibifu wa mazingira ya mpango wa
mfuko wa uzazi na hasa kwa uchokonoaji wa mimba, hivyo kufungwa kwa
kizazi, pengine hedhi inakoma na kwa kutopata hedhi wanawake wengi
huchanganyikiwa.
Tatizo hili la ugumba huwa linasababishwa na kukwanguliwa kwa ile ngozi
laini inayozunguka tumbo la uzazi. Kukwanguliwa huko kunatokana na ama
vifaa vinavyotumiwa kuichokonoa mimba hiyo au madawa makali.
Athari nyingine kama uchokonoaji umepita kiasi na kufikia kwenye utumbo
mkubwa huathirika na kusababisha utumbo kutobolewa na kuwekwa mrija wa
kutolea choo kikubwa.
Vile vile hali hiyo usababisha ugandaji wa damu kwenye mishipa ya fahamu
kuelekea kwenye ubongo. Hii ni hatari mno, kwani inasababisha mhusika
kuwa na hali kama ya kiharusi.
Kutokana na athari hizo na hasa ugumba, wanawake hupatwa na msongo mzito
wa mawazo na kuchanganyikiwa kisaikolojia, hivyo huanza kuwa na tabia
za ajabu za hasira na hata chuki kwa wenzao wenye watoto na hata
kuwachukia watoto wa wenzao pasipo sababu za msingi. Wanajihisi wamekosa
ule ubora wa kuitwa mwanamke.
Hapa nchini, sheria inayoruhusu kutoa mimba haipo, hivyo jambo hili ni
kosa na hivyo hufanywa kwa kificho, pengine katika mazingira yasiyofaa,
kukosa ujuzi wa kitaalamu na vifaa visivyo sahihi.
Wakati mwingine ni wasichana wenyewe hushawishiana jinsi ya kutoa mimba
na kusasabisha madhara yote haya. Inabidi kuchukua hatua nax kuacha
kabisa
Baadhi ya wasichana baada ya kukumbwa na tatizo la ugumba hujifariji
kuwa ati wamebaki na uzuri wao na hapo hujiingiza kwenye biashara haramu
ya kuuza miili yao na kujiweka kwenye hatari ya maambukizi ya magonjwa
ya ngono na kupata ukimwi pia.
Kutoa mimba huleta ulemavu wa maisha, kutokuzaa kabisa na ni kifo. Natoa
rai kwa wanawake wote waachane na tabia hiyo ya kuzichokonoa mamba, na
waachane na kubeba mimba wasizozipanga, pia waepuke tamaa za maisha ya
starehe kwani zinawatumbukiza kwenye majanga.
WATOTO WANAHAKI YA KUISHI, KUTOA MIMBA NIKOSA LA JINAI.