
Sasa ni dhahiri shahiri wanahabari wengi makanjanja wamekuwa na maisha
magumu sana kwani wengi walitegemea kuishi kwa kuwasifia 'wanasiasa' na
'wapiga dili'. Mathalani, Ma-don wakubwa wa unga,makontena nk walikuwa
wanamiliki kundi la waandishi wa habari wenye lengo moja kuu tu
'kuwasafisha'.
Hali imegeuka, magenge mengi yameyeyuka huku wakiwaacha vijana wao
(waandishi makanjanja) wasijue cha kufanya. Kundi kubwa la makanjanja
kwa sasa limegeukia mitandao ya kijamii kutengeneza akaunti feki zenye
mrengo wa kupotosha. katika pitapita zangu nimekutana na baadhi ya
wahariri ambao kabla ya Manji kubanwa walikuwa wenye 'fujo' nyingi mjini
lakini ghafla hali yao imedhohofu. Udhibiti wa posho kwa wanasiasa pia
umesababisha waandishi wengi kukosa ujira kwani hakuna mwanasiasa
anayemudu kubeba waandishi kwa kukosa pesa za kuwalipa.
Magazeti mengi yaliyotamba miaka mitano iliyopita yamekufa au yanatoka
mara moja moja sana, huku gazeti la Jamvi la habari likitokomea
kusikojulikana.
Ushauri wangu ni kwamba kundi hili la 'wapambe' na 'makanjanja' wa
habari sasa waelekeze nguvu zao katika mambo yenye tija kwa ajili yao
binafsi na kwa taifa kwani kwa sasa hata zile kurasa zao maarufu zenye
kukejeli serikali katika mitandao ya kijamii zimedorora.
Heshima imerudi mjini.
Credit - Jf
Tags
RAIS MAGUFULI