
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uganda jana wamesaini
mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga
Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Yoweri Museveni ikulu jijini Dar
es salam.
Akizungumza baada ya kutia saini tamko hilo Mhe. Rais Magufuli
amemshukuru Mhe. Rais Museveni kwa hatua ambayo Tanzania na Uganda
zimefikia katika mradi wa bomba la mafuta la Hoima – Tanga na ameeleza
kuwa mradi huo ni matokeo ya urafiki na undugu wa kihistoria uliopo kati
ya nchi hizi mbili.
“Kwa hiyo mimi nakushukuru sana Mhe. Museveni na kwa niaba ya Watanzania
wote tumefurahi sana, umetengeneza historia ya Tanzania na Uganda na
pia umeimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu,
Watanzania hawatakusahau” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wa Rais Museven ambaye ni mmoja wa wafuasi wa Baba wa Taifa
Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi
mbalimbali za Afrika na aliyekuwa na ndoto ya kuiunganisha Afrika nzima
zao ili kujipatia manufaa ya kiuchumi, ametoa wito kwa viongozi hasa
vijana kuendeleza misingi ya umoja na ushirikiano kati ya nchi hizo
mbili.
"Nimefurahi sana leo, najua kuna kazi kubwa imefanyika hadi kufikia
hatua hii, lakini hii pia imeonesha kuwa na sisi tunaweza” amesema Mhe.
Museveni.
Tanzania na Uganda (Inter-Governmental Agreement–IGA) ambao umepangwa
kukamilika katika kipindi cha wiki moja, na baada ya hapo taratibu za
kuweka jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zitafanyika.
Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima – Tanga wenye urefu wa
jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya
Tanzania utagharimu Dola za Marekani Bilioni 3.55, unatarajiwa
kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi
unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000.
Tags
mkataba