Kamati ya Saa 72
imekaa kupitia mambo mbalimbali na moja ya uamuzi wake ni kuhusiana na
wachezaji wa Yanga kumuangusha mwamuzi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu
Bara dhidi ya Mbao FC na imewamua kuwasimamisha kuitumikia Ligi Kuu
BAra.
Wachezaji Deus
Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wa Yanga wamesimamishwa kucheza
mechi za Ligi Kuu wakati wakisubiri suala lao la kumsukuma na
kumwangusha Mwamuzi Ludovic Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Walifanya kitendo
hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati umezingatia
Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.
Mwamuzi Ludovic
Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi dhidi
yake ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa
Waamuzi.
Tags
MICHEZO