Kila mtu huhitaji kuwa mwenye nguvu na mchangamfu kila siku ili kuweza
kuendelea kufanya shughuli za uzalishaji mali za kila siku.
Lakini tatizo linakuja pale ambapo kila siku utajikuta ukiamka ukiwa
mchovu na usiyetamani kufanya chochote kabisa zaidi ya kukaa tu.
Hata hivyo ni vyema ikafahamika kuwa unapokumbwa na hali hiyo basi huwa
kuna sababu na zifuatazo ni baadhi tu ya sababu ambazo huweza kumfanya
mtu kuhisi uchovu.
Upungufu wa damu (anemia)
Upungufu wa damu ni mojawapo ya chanzo cha mtu kuweza kuhisi hali ya uchovu wa mara kwa mara hususani kwa wanawake,
Ikiwa unapata muda mzuri wa kutosha na unapata virutubisho vyote muhimu
na bado unapatwa na hali ya kuhisi uchovu basi ni vyema uende ukafanye
uchunguzi kuona kama hauna tatizo la anemia.
Tatizo la upungufu wa damu mwilini ni rahisi sana kukabiliana nalo
ambapo mgonjwa atatakiwa kupata virutubisho na vyakula vyenye madini
chuma ndani yake.
Kisukari (Diabetes)
Kuhisi uchovu wa kila siku na mara kwa mara huweza kuwa ni kiashiria cha
ugonjwa wa kisukari. Hivyo ikiwa unahisi hali hiyo kila siku na unapata
haja ndogo mara kwa mara na uoni wako unakuwa hafifu basi unaweza
kuonana na wataalam ili kufanya vipimo zaidi.
Magonjwa ya moyoKama unapata uchovu wa mara kwa mara huenda ikawa ni
dalili ya matatizo ya moyo, hivyo pia ni nzuri ukaonana na wataalam kwa
ajili ya uchunguzi zaidi.
