
Zabibu hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa
kama tunda na tunda hili hukuwa katika kichana chenye zabibu 6 hadi
300.
Matunda haya inaelezwa kwamba yalianza kulimwa huko nchini Uturuki,
lakini kwa hapa kwetu nchini yanapatikana sana mkoani Dodoma.
Matunda haya huwa na rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza ,
njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba hapa kwetu Tanzania wengi
tumezoea yale ya rangi nyeusi.
Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi na nzuri zaidi kutokana na
uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu
hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.
Pia zabibu husaidia damu kuwa nyepesi na kuifanya isigande ndani ya
mishipa ya damu, hivyo mtumiaji wa zabibu hupunguza hatari ya kupata
kiharusi (stroke)
Tunda hili pia husifika kwa kutibu tatizo la upungufu wa damu, hususani
kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na
ugonjwa wa bawasili pia.
Hali kadhalika zabibu pia husaidia katika tiba na kinga dhidi ya
magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa
kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.
Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili
hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu
maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.
Sambamba na hayo, juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo
kufanya kazi kwa ufasaha zaidi na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini
pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa
kumeng’enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.
Lakini pia kutokana na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai
kuwa ni dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na
kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect)
Hizo ndio baadhi ya faida za zabibu ambazo mtumiaji huweza kuzipata pale anapotumia tunda hili mara kwa mara.