
Watu husema hakuna kinachozidi upendo wa mama na wengi wao
wamedhihirisha hilo kama ilivyokuwa kwa Seneta wa Australia, Larissa
Waters ambaye aliamua kumnyonyesha mtoto wake wa miezi miwili akiwa
bungeni.
Waters ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa wa kwanza kufanya hivyo nchini humo.
Hata hivyo Bunge la nchi hiyo liliruhusu kunyonyesha lakini tangu lilipotoa ruhusa hiyo hakuna mbunge aliyewahi kufanya hivyo.
Waters amewatia moyo wanawake kwa kusema kuwa wanataka wanawake wazazi
wengi zaidi bungeni kwa sababu hakuna shaka juu ya kunyonyesha mtoto.
Tags
Bunge la Nje