Meya wa jiji la Dar es Salaam
Isaya Mwita mwenye kofia katikati akizungumza jambo na Mwanaharakati wa
kipindi cha Wanawake Live Joyce Kiri wa kwanza kulia , wakati wa
ufunguzi wa semina ya vikundi vya wakina mama vya wanawake Live
iliyofanyika Pugu jijini hapa leo.kushoto ni Diwani wa kata ya
Pugu Henry Kilewo
CHRISTINA MWAGALA,OFISI YA MEYA WAJIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita amesema anatambua mchango mkubwa unaotokana na wakina
Mama na hivyo kuwataka wa kina Baba kuwaunga mkono kwa asilimia 100
katika shuguli za maendeleo.
Meya Mwita alitoa kauli hiyo jiji
hapa jana wakati wa uzinduzi wa Vikundi vya wa kina mama vya wanawake
Live yaliyofanyika Pugu halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Meya Mwita alisema wakina mama
ndio msingi mkubwa ndani ya familia , Taifa kutokana na mchango ambao
huutoa jambo ambalo linaleta ustawi mkubwa maendeleo.
Aliongeza kuwa licha ya
changamoto ambazo hukutana nazo lakini wamekuwa ni watu wasio kata
tamaa hivyo akasisitiza kuwa wakina baba wanatakiwa kutoa ushirikiano
wao kwa silimia 100.
Aidha Meya Mwita aliwapongeza wa
kina mama kutokana na ubunifu waliokuwanao kila kukicha katika
kujitafutia maendeleo na hivyo kuwa msaada mkubwa ndani ya familia zao
ikiwemo kuwasaidia majukumu wakina baba.
“ Natambua mchango wenu sana,
mmekuwa wabunifu , mnajishugulisha kwenye mambo mbalimbali ya
kimaendeleo, mmekuwa mstari wa mbele kutengeneza miradi ambayo inasaidia
kwenye familia zenu bila hata wakina baba kushiriki.
“ Hivi sasa mmeanzisha vikoba, hii
yote ni katika kujituma kwenu ili muondokane na umasikini, nawapongez
sana” alisema Meya Mwita.
Akizunguzungumzia changamoto
zilizopo kwenye dampo, la Pugu Kinyamwezi, Meya Mwita alisema wameanza
kuandaa utaratibu ambao utawasaidia kuondokana na chagamoto hizo.
Alisema suala la dampo limekuwa ni changamaoto kubwa lakini hadi kufikia Agosti mwaka huu, uratibu huo utakuwa umeshatolewa.
Akizungumzia suala la maji ,
alisema kuwa Kata ya Pugu imekuwa na changamoto hiyo na hivyo kuwa kero
kwa wakina mama lakini kwa sasa upo mpango wa kuwawezesha kupata visima
vitatu vya maji.
Alisema kwenye shuguli za
maendeleo hakuna mambo ya vyama na kwamba viongozi walipo kwenye nafasi
zao wanatakiwa kuwatumikia wananchi wote ili kuhakikisha kwamba wanapata
maendeleo waliyoahidiwa.
“ Kwenye maendeleo hakuna mambo
ya vyama, kila mmoja anahitaji maendeleo, mambo ya vyama hivi sasa
tunayaweke kando, ili kupata muda wa kufanya kazi moja tu,
yakuwatumikia wananchi ambao mmetuchagua” alisistiza.
“ Ndani ya jiji hili tunataka
kuleta maendeleo, ili mwaka kesho nikija kusimama hapa yale ambayo
tunayazungumzaleo, tusiyarudie tena na badala yake tuzungumze mambo
mengine.B
Tags
MEYA DAR