Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23
za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa pili kulia) akieleza kuwa
Tanzania inakua kwa kasi kiuchumi jambo ambalo linawavutia viongozi
wengi kufuatilia kwa karibu maendeleo yake, alipokutana na Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), katika
Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiongoza Mkutano
kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (mbele
kulia) ambapo alisema mahitaji makubwa wa nchi ni maendeleo ya kilimo na
upatikanaji wa nishati ya umeme ili viweze kuchochea uchumi wa viwanda.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba ( kulia)
wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao uliohusu suala
la Uchumi katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es
salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (watatu kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (wa tatu
kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Maafisa waandamizi
wa Wizara hiyo baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu hali ya uchumi
katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano kati
ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (hayupo
pichani) wakimuaga baada ya kumalizika kwa Mkutano katika ukumbi wa
Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Tags
MIFUGO/KILIMO/UVUVI