
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Mwakyembe amewasihi
watanzania kuacha kutumiwa na viongozi mbalimbali kwa kuimba nyimbo za
masuala ya kisiasa na badala yake wafanye kazi ambazo zitawasaidia
kupata mafanikio.
Waziri Mwakyembe aliyasema hayo bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali
zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya wizara
yake.
"Tembea dunia kote huko, nimekwenda Nigeria na kuona wasanii wakubwa
kama Tiwa Savage, Don Jazz, Akon, P Square wale hawaimbi kuhusu viongozi
wao wa kisiasa.
"Hivyo niwasihi wasanii wangu, muache kuimba kuhusu siasa sababu hii ni
‘entertainment industry’ (sekta ya burudani) na sio ya masuala ya
kisiasa, "alisema Waziri Mwakyembe.
Aidha, waziri alisema kama kuna msanii yeyote anayetaka kuwa mwanasiasa
aache muziki akagombee udiwani kwani wasanii waliotaka kuchanganya siasa
na muziki walipotea kabisa.