Baadhi ya wananchi wa
kijiji cha Ikungi waliohudhuria mkutano maalum wa kijijji hicho
wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani.
Mkuu wa wilaya ya
Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi hawapo pichani kwenye
mkutano maalum wa kijiji cha ikungi,kulia kwake ni kaimu mwenyekiti wa
kijiji hicho Athuman Seleman na kushoto kwake ni kaimu mkurugenzi wa
halmashauri Haika Massawe.
Mkaguzi wa ndani wa
halmashauri ya Ikungi Kitundu Mkumbo akisoma taarifa ya ukaguzi mbele ya
mkutano maalum wa kijiji cha Ikungi.
………………………………………………………………….
MKUTANO maalum wa
Kijiji cha Ikungi wilayani Ikungi mkoani Singida umemuondoa Mwenyekiti
wa kijiji hicho Hussein Ikusi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka
kwa kufanya ubadhirifu wa mali za kijiji zenye thamani ya shilingi
milioni 9.
Ubadhirifu huo
aliufanya toka alipoingia madarakani mwaka 2014 akishirikiana na
aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji
cha Irisya.
Hayo yalibainika baada
ya halmashauri ya kijiji kuitisha kikao maalum tarehe 24 aprili mwaka
2017 wakimtuhumu mwenyekiti kwa hoja zipatazo 5.
Hoja hizo ni kushindwa
kusimamia mali za kijiji,kushindwa kusimamia mipaka ya kijiji,kushindwa
kuonyesha ushirikiano na uongozi wa halmashauri ya wilaya,Ofisi ya mkuu
wa wilaya na taasisi za serikali zilizopo wilayani,kuwa chanzo cha
migogoro badala ya kuwa mtatuzi na kushindwa kusimamia usomaji wa mapato
na matumizi ya kijiji kwa mujibu wa sheria kwa kipindi cha miaka
miwili na nusu.
Ubadhirifu huo
umebainishwa na mkaguzi wa mahesabu ya ndani Kitundu Mkumbo aliyeagizwa
na mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu kufanya ukaguzi wa mapato na
matumizi ya kijiji baada ya kupokea tuhuma kuhusiana na mwenyekiti huyo.
Akizungumza katika
kikao cha kutoa taarifa kuhusiana na maamuzi yaliyoafikiwa na
halmashauri ya kijiji Mtaturu alimuagiza kaimu mkurugenzi wa
halmashauri Haika Massawe kumsimamisha kazi mtendaji wa kijiji cha
Irisya Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji kingine ili arudi ikungi
kujibu tuhuma za kuondoka na vitabu 12 vya kukusanyia mapato
alivyoshindwa kukabidhi wakati anahama ikiwemo na kutoa maelezo ya
fedha zilizoonekana kupotea mikononi mwake.
“Bwana Ikusi kabidhi
fedha na mali kama ushauri wa mkaguzi wa mahesabu alioutoa hapa mbele ya wananchi”alisisitiza Mtaturu.
fedha na mali kama ushauri wa mkaguzi wa mahesabu alioutoa hapa mbele ya wananchi”alisisitiza Mtaturu.
Aprili 24 mwaka huu
halmashauri ya kijiji iliazimia kwa kauli moja kumuondoa mwenyekiti
huyo kutokana na tuhuma hizo dhidi yake huku huku ikisisitiza kuwa
Usimamizi wa Rasilimali za Umma ni mabadiliko Chanya kwa maendeleo ya
Ikungi.
Tags
WENYEVITI WA MITAA