
MAMLAKA ya MapatoTanzania (TRA) imetangaza mkakati wa kuanza kuwasajili
wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga ili waweze kutambulika na
kurasimishwa rasmi.
Mkurugenzi wa Elimu Kwa Walipa Kodi, Richard Kayombo, akizungumza katika
semina ya waandishi wa habari jana amesema wamachinga baada ya
kutambuliwa watawekewa utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao na
kuchangia mapato Kwa serikali.
Kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), amesema TRA haitozi Kodi Kwa
mizigo inayosafirishwa kwenda nje ya nchi badala yake mizigo hiyo
inatozwa Kwa huduma zinazofanyika nchini.
Mada zilizojadiliwa ktk semina hiyo ni Kodi ya Majengo na elimu ya Kodi Kwa anayeanza biashara.