• Mwanzo
  • About Us
  • Contact Us
BANDA MEDIA BLOG
  • MWANZO
  • HABARI
  • _SIASA
  • _MAISHA
  • _JAMII
  • _TEKNOLOJIA
  • MAGAZETI
  • SIASA
  • _KITAIFA
  • _KIMATAIFA
  • MICHEZO
BANDA MEDIA BLOG
HomeEBOLA RUKWA

RC afanya ziara ya siku tatu kuongea na viongozi na wananchi wanoishi mipakani ili kujihadhari na Ebola

byJohn Banda -Tuesday, May 30, 2017
0

 
Zelote Stephen [RC  RUKWA]

Katika kuhakikisha Mkoa wa Rukwa Upo salama kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yatakayoweza kujitokeza, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amefanya ziara ya siku tatu katika mwambao wa ziwa Tanyangika kwenye Kata ya Kirando, Kabwe na Kasanga vijiji ambavyo ni jirani nan chi jirani ili kujionea namna Halmashauri ya Nkasi na Kalambo namna zilivyojipanga kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hautii mguu katika Mkoa na nchi kwa ujumla.


Ziara hiyo aliianza siku ya Ijumaa tarehe 26 hadi 28. 05. 2017 mara baada ya kumaliza kumalizika kwa mafunzo ya siku tatu yaliyohusu utumaji wa taarifa za magonjwa kwa kieletroniki (e-idsr) yenye kusisitiza tahadhari ya ugonjwa wa ebola uliopo katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya wa Serikali na Sekta binafsi kwa Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga vijijini.

Mafunzo ya awamu ya pili yanatarajiwa kumalizika tarehe 31. 05. 2017 kwa Halmashauri za Kalambo na Nkasi ikiwa ni muendelezo wa awamu ya kwanza kwa Halmashauri ya Sumbawanga Vijijini na Manispaa ya Sumbawanga yaliyoisha tarehe 26. Mwezi wa tano.

Ili kujiridhisha na maandalizi ya Halmashauri zinazopakana na nchi za jirani yaani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na Zambia Mkuu wa Mkoa alipita katika bandari maarufu za pwani ya ziwa Tanganyika na kuongea na vyombo vya usalama ikiwemo uhamiaji, Sumatra, TRA, jeshi la polisi, jeshi la wananchi, maafisa forodha pamoja na maafisa afya kutoka Wilayani.

Pia Mh. Zelote aliongea na viongozi wa serikali za vijiji na kata wakiwemo madiwani, watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji, maafisa ugani wa kata na vijiji, maafisa afya wa kata na vijiji na kufanya mikutano ya hadhara ili kuwapa wananchi ujumbe aliokwenda nao katika kuhakikisha ugonjwa huo haunusi katika mkoa wa Rukwa na nchi ya Tanzania.

Pamoja nae Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu, Mratibu wa Chanjo Mkoa Gwakisa Pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Afya wa usimamizi na ufuatiliaji Solomon Mushi, Mkuu wa Wilaya, makatibu tawala wa wilaya pamoja na kamati za ulinzi na usalama za Wilaya.

Katika kila Wilaya aliyopita Mh. Zelote alihakikisha anapewa taarifa za maandalizi ya Wilaya na kisha kwenda kwenye mipaka ili kujionea kwa macho yake maandalizi hayo na pia kuongea na wananchi wanoishi karibu na mipaka hiyo.

Wakati akiwa kwenye ziara hiyo Mh. Zelote alikuwa akisisitiza utayari pamoja na kujihadhari kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata na pia kwa vyombo vya usalama vya maeneo hayo ya mipakani.

Katika suala la utayari Mh. Zelote Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya athari ya ugonjwa huo na namna ya kujikinga nao ikiwa ni pamoja na kuelezwa dalili za ugonjwa na njia za maambukizi ya ugonjwa huo na kuwasisitiza wananchi kwenda zahanati pindi wanapojiskia kuumwa na sio kukimbilia kwenye maduka ya dawa na kuagiza vidonge bila ya kujua ugonjwa anaoutibu.

Pia katika kusisitiza hilo Mh. Zelote aliwasihi wananchi kutokimbilia kwa waganga wa kienyeji pindi wanapoumwa na badala yake wakimbilie kwa wataalamu wa afya kwenye zahanati ama vituo vya afya. Na kuwaonya kuwa kupitia hizi taarifa za ugonjwa wa ebola kunaweza kukajitokeza matapeli ambao watajitangaza kuutibu ugonjwa huo jambo ambalo si kweli, hivyo aliweka msisitizo kuwa ugonjwa wa Ebola hauna Tiba.

“Mtu yeyote atakayejiskia vibaya basi haraka akimbilie kwenye zahanati ama kituo cha afya na sio kwa mganga wa kienyeji, na mjiepushe mbali  sana na matapeli wanaotibu watu vichochoroni ama wanaosema dawa ya Ebola ipo,…. Hakuna,” Mh. Zelote alieleza.

Pamoja na hayo Mh. Zelote alionya kuwa katika kusimamia jambo hilo hatakuwa na utani, dhihaka ama masihara kwayeyote atakaekiuka taratibu zilizowekwa ili kujihadhari na ugonjwa huo kuingia katika mkoa wa Rukwa.

“Mimi nafahamu kwamba watu wanaoishi humu kwenye mipaka wameoa ama kuolewa katika nchi za jirani, na kwamba watanzania utamaduni wetu ni ukarimu kwa wageni lakini katika hili tupunguze ukarimu mpaka jambo hili liishe, na yeyote atakayegundulika anamhifadhi mgeni kinyume na taratibu, huyo ni mhalifu,” Mkuu w Mkoa alisema.

Katika kuonesha athari kubwa inayoweza kupatikana endapo uginjwa huo utapenya katika nchi yetu Mh. Zelote alieleza kuwa gharama za kumshughulikia mgonjwa mmoja ni kubwa sana na kuongeza kuwa endapo ugonjwa huo unathibitishwa kwenye nchi Fulani basi tatizo hilo si la nchi hiyo tu ni la dunia nzima.

“Nguo inayotumika kumshughulikia mtu mmoja inauzwa milioni 10 na kwa wenzetu huko afrika ya magharibi Ivory Coast ambako walikumbana nao watu 11,000 walifariki, wakiwemo madaktari ambao walikuwa wakiwauguza wagonjwa, mtu mmoja tu akiupata basi kijiji kizima kinafungwa hakuna mtu kuingia katika kijiji hicho wala kutoka,” Mh. Zelote alisisitiza.

Lakini pia aliwatoa hofu wananchi na kuwaambia kuwa mpaka sasa Tanzania hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola.

Nae Daktari wa Mkoa Dkt. Kasululu alisema kuwa tangu ugonjwa huo kutolewa taarifa na Wizara ya Afya tarehe 12. 05. 2017 watu watatu wlikuwa wamefariki na wengine 12 walikuwa wako chini ya uangalizi lakini hadi kufuikia tarehe 25. 05. 2017 idadi ya wagonjwa iliongezeka hadi kufikia wagonjwa 45 na kuongeza kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kadiri siku zinavyokwenda mbele.

“Idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeak kila kukicha hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunajiandaa na kujihadhari kweli, maana wagonjwa hawa wapo kwenye misitu ambapo usafiri wa kawaida haufiki isipokuwa Helkopta na pikipiki, hivyo wagonjwa wanaweza kuwa wengi na bado hawajajulikana,” Dkt Kasululu alisisitiza.

Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Dk. Makundi Maige alielezea mikakakti ya Halmashauri ya Nkasi namna ilivyojipaga kuhakikisha wanakaa mbali na ugonjwa hatari wa Ebola.

“ Wilaya imeainisha kata tatu za Kirando, Kabwe na Wampembe ambazo zimetengwa kwaajili ya kupokea wageni kutoka nchi za jirani, tukifahamu kuwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyia kuna Kata 10 ambazo ugonjwa huu unaweza kuingia kwa urahisi, ambazo ni Kabwe, Kirando, Wampembe, Itete, Kipili, Mkinga, Korongwe, Ninde, Kizumbi na Kala,” Dk. Makundi aliainisha.

Katika kubainisha upokezi wa wageni hao Dk. Makundi alisema kuwa kituo cha Wampembe kitapokea wageni wanoelekea kijiji cha Kilambo hadi Msamba, Kituo cha Kirando kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Ninde hadi Kazovu na kituo cha Kabwe kitapokea wageni wanaoelekea kijiji cha Utinta hadi Kalila.

Na kuongeza kuwa wageni wote kutoka nchi za jirani watalazimika kupitia katika vituo hivyo na sio kuingia kiholela kama ilivyozoeleka na kabla ya kuendelea na safari zao watakuwa wakichunguzwa afya zao.

Kwa kuzingatia namna ugonjwa huo unavyoenea Wilaya imetenga eneo maalum kwaajili ya matibabu ili kuepuka kuchanganya wagonjwa watakaobainika kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.

Pamoja na hayo Wilaya imejipaga kuzizungukia kata zote 10 na kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa maeneo hayo, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha viongozi wa dini, wazee maarufu, vijana, waalimu na wanafunzi juu ya ugonjwa huo hatari.

Nao upande wa Wilaya ya Kalambo  walieleza mipango yao juu ya udhubiti wa ugonjwa huu, ambapo mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Alcado Mwamba aliweza uainisha tahadhari mbalimbali ambazo Wilaya imezichukua kuhakikisha wanaudhibiti ugonjwa huo kutokuingia katika Wilaya hiyo.

Miongoni mwa tahadhari walizochukua ikiwa ni kuwasambazia wananchi vipeperushi vyenye kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola lakini pia kuihamasisha jamii kutoa taarifa haraka kwa uongozi wa serikali pindi tu wakibaini kuna mgeni aliyeingia kinyume na taratibu zilizowekwa.
 

 Afisa Habari - Mkoa wa Rukwa.








Tags EBOLA RUKWA
  • Facebook
  • Twitter

You may like these posts

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG

LIFE SHINING BIBLE COLLEGE

BANDA MEDIA BLOG

IPAGALA , DODOMA

Tufuate Mtandaoni

JOHN BANDA

BANDA MEDIA BLOG

WALIOTUTEMBELEA

TUWASILIANE HAPA

ZINAZOSOMWA ZAIDI

MAGAZETI YA LEO

HIZI HAPA KURASA ZA MBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO, MEI 12, 2026

byJohn Banda-Tuesday, May 12, 2026

TAARIFA MUHIMU KUTOKA JWTZ LEO

Sunday, May 10, 2026

HIZI HAPA KURASA ZA MBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO, MEI 11,2026

Monday, May 11, 2026

RAIS SAMIA AMEFANYA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA MICHEZO – DKT. MWIGULU

Sunday, May 10, 2026

KADRI BINADAMU ANAVYOPATA MAENDELEO NDIVYO ANAVYOJIVIKA UKICHAA- DKT GWAJIMA

Monday, May 11, 2026

HIZI HAPA KURASA ZA MBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO MEI 14,2026

Thursday, May 14, 2026

HIZI HAPA KURASA ZA MBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO, MEI 10,2026

Sunday, May 10, 2026

KAIRUKI ASISITIZA MALEZI BORA HUKU DOKTA KWEKA AKIONYA MADHARA YA SHISHA

Sunday, May 10, 2026

WAZAZI WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI NA ELIMU YA WATOTO

Sunday, May 10, 2026

MWENYEKITI BODI YA REA ATOA WITO KWA WANANCHI KULINDA MIUNDOMBINU YA UMEME

Monday, May 11, 2026

BLOGU MARAFIKI

  • MICHUZI BLOG
    TANZANIA NA MAREKANI KUIMARISHA MAHUSIANO KWENYE SEKTA YA AFYA - Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Mei 14, 2026 amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Andrew Lentz na kufanya majadiliano kuhusu Mkataba ...
    6 hours ago
  • Wazalendo 25 Blog
    Muungano : Ubalozi wa Tanzania Zimbabwe Waadhimisha Miaka 62 ya Muungano wa Tanzania. - Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zimbabwe umeadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hyat...
    1 week ago
  • ShaffihDauda.co.tz – Gambling News
    Global Gaming Report: Markets, Enforcement, and Compliance - If you’re navigating today’s global gaming market, you know the stakes keep rising alongside the industry’s value. With compliance demands tightening and e...
    2 weeks ago
  • PAMOJA BLOG
    TCAA Yatoa Msaada kwa Kituo cha Tupendane Dodoma - Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, imetoa msaada katika kituo cha kulelea watoto cha Tupendane kilichopo ji...
    3 weeks ago
  • Official - Millard Ayo Website
    Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...
    1 year ago
  • KAZENZELE
    TBA WANAFUATILIA KUJIRIDHISHA JUU Y AMAJENGO HAYA - Wakati picha za majengo yenye nyufa zikisambaa mitandaoni ikidaiwa ni ya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), uongozi wa Wakala wa Majengo ...
    8 years ago

KUMBUKUMBU

  • 2015 (694)
  • 2016 (3127)
  • 2017 (4025)
  • 2018 (444)
  • 2022 (1117)
  • 2023 (246)
  • 2024 (2866)
  • 2025 (718)
  • 2026 (930)

TAFSIRI YA LUGHA

MAKTABA YETU

  • SIASA
  • MAGAZETI YA LEO
  • HABARI
  • AFYA
  • MICHEZO
  • KIMATAIFA
  • ELIMU
  • MAHUSIANO
  • BIASHARA
  • UTALII
  • Burudani
  • UTAMADUNI
  • HISTORIA
  • KITAIFA
  • maisha
  • Uchumi
  • Mahakama
  • SHERIA
  • Samia Hassan Suluhu
  • AJIRA
  • UTEUZI
  • KILIMO
  • Zanzibar
  • Dini
  • RUSHWA
  • makala
  • UBUNIFU
  • Uchaguzi
  • TEKNOLOJIA
  • kanisani
  • RIADHA
  • TENDO LA NDOA
  • WAHARIRI

HABARI ZA KALE

  • HUU HAPA WASIFU WA DKT. NEEMA MAJULE MGOMBEA UBUNGE KUPITIA UWT DODOMA
     DR NEEMA PETER MAJULE Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake  Mkoa Dodoma Wasifu Mwenyekiti wa UWT Mkoa Awamu 2 Mchumi na mtaalum wa maandiko ...
  • TANGAZO LA AJIRA ZA KAZI 1,150 NCHINI QATAR
     
  • ROSE MUHANDO KUOLEWA NA ASKOFU MKENYA
      MALIKIA wa nyimbo za injili Nchini Tanzania Rose Muhando anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni huko nchini Kenya na  mwimbaji mwenzake wa ...
  • HII HAPA SIMULIZI YA MWALIMU ''SINGLE MOTHER'' ALIYEKIMBIA KAZI KISA NGONO
                                Mwalimu Doris Peter akiwa kwenye majukumu yake UALIMU ni wito, pia ni kazi kama zilivyo kazi nyingine za kitaa...
  • HIZI HAPA KURASA ZAMBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JULAI 9,2025
                                                 
  • DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI
      Mwanaume nisikilize! Umasikini unauma zaidi ukiwa mwanaume. Familia inakutazama tofauti sana hata kama haikuambii ila we fahamu tu kuwa ku...
  • WAGOMBEA WA CCM KATIKA NAFASI ZA UBUNGE, UWAKILISHI, VITI MAALUM NA UDIWANI SOMENI HII
               
  • WAUMINI WAMPELEKA PADRI KITIMA VATIKANI, WAOMBA UCHUNGUZI WA MWENENDO WAKE
    Dar es Salaam, 22 Desemba 2025. Waumini wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, Stanslaus Thobias Nyakunga na Elia Phaustine Kabote, wamewasilis...
  • HIZI HAPA KURASA ZA MBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO, MACHI 18,2026
     
  • KUDHURUMIWA MALI KWA WAJANE BAADA YA KUFIWA NA WAUME ZAO KWASABABISHA SIMANZI...
    Mwenyekiti wa Jukwa la Uwezeshaji Kiuchumi Mkoa wa Dodoma, Mary Mabara, akielekeza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wanawake wa jana wa...
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG

HABARI MCHANGANYIKO

HUU HAPA WASIFU WA DKT. NEEMA MAJULE MGOMBEA UBUNGE KUPITIA UWT DODOMA

Wednesday, July 16, 2025

TANGAZO LA AJIRA ZA KAZI 1,150 NCHINI QATAR

Sunday, February 01, 2026

ROSE MUHANDO KUOLEWA NA ASKOFU MKENYA

Wednesday, January 14, 2026

HABARI MPYA

ZINAZO BAMBA ZAIDI

HIZI HAPA KURASA ZA MBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO, MEI 12, 2026

Tuesday, May 12, 2026

TAARIFA MUHIMU KUTOKA JWTZ LEO

Sunday, May 10, 2026

HIZI HAPA KURASA ZA MBELE NA NYUMA KWENYE BAADHI YA MAGAZETI YA LEO, MEI 11,2026

Monday, May 11, 2026

Copyright © 2015 - 2026 Banda Media Blog All Right Reserved

Developed by Gadiola Emanuel
Theme by AP | Developed by Gadiola Emanuel
  • Home
  • About Us
  • Contact Us
  • News

Contact Form