Timu ya soka ya taifa
ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti imeanza vizuri michuano ya Kombe
la Mataifa Afrika baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya mabingwa
watetezi wa michuano hiyo, Mali.
Boys walionyesha
kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu huku wakijilinda katika kila idara
katika mechi hiyo ya Afcon, michuano inayofanyika nchini Gabon.
Mashambulizi ya Boys
yalikuwa ni yale ya kushitukiza lakini wakatumia muda mwingi kujilinda
kwa mipango dhidi ya Mali ambao wachezaji wake walikuwa na maumbo
makubwa zaidi.
Sare hiyo, inaifanya Serengeti kuanza vizuri michuano hiyo ikiwa imekujikusanyia pointi ya kwanza.
Tags
SERENGETI BOYS