Waziri wa Katiba na Sheria wa
Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa
Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari
ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya
Serena, Kampala, Uganda
Waziri wa Katiba na Sheria wa
Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa
Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari
ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya
Serena, Kampala, Uganda
Ujumbe wa Tanzania na Uganda
ukishuhudia tukio la utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa
Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga
nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena,
Kampala, Uganda.
Waziri wa Katiba na Sheria wa
Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi, akihutubia baada ya kutia saini
Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini
Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo
katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Tanzania, Bw. George Masaju (kulia) na Mwanasheria wa Uganda Bw. Milliam
Byaruhanga (kushoto), wakionesha nakala za Mkataba wa Ujenzi wa Mradi
wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya
Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena,
Kampala, Uganda.
Waziri wa Katiba na Sheria wa
Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa
Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakionesha Mkataba wa Ujenzi wa Mradi
wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya
Tanga nchini Tanzania, baada ya kuusaini, tukio lililofanyika leo katika
Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
(Picha na Wizara ya Fedha na Mipango)
……………………………………
Na Benny Mwaipaja, WFM
Serikali za Tanzania na Uganda
zimetiliana saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la
kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania lenye urefu wa
Kilometa 1,443, uliokadiriwa kugharimu zaidi ya Dola bilioni 3 nukta 55,
mjini Kampala Uganda, leo.
Mkataba huo umesainiwa na Waziri
wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi na Waziri wa
Nishati wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Tukio hilo limekuja siku chache
baada ya Marais wa Nchi hizo mbili, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa
Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni, kutia saini tamko la pamoja la
kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba, Ikulu Jijini Dar
es salaam.
Hafla ya kutia saini Mkataba huo
iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala, Uganda
imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo
Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na
Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi
kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia kusisimua uchumi wa
nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya watu 10,000
wanatarajiwa kunufaika na ajira.
Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliuelezea mradi huo
kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya mafuta katika
eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba Tanzania
inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo
yatapitishwa katika bomba hilo hilo.
Tags
Tanzani/ Uganda