Mwanasheria
na Msimamizi wa Mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi
wa nyumbani nchini Tanzania, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye
semina kwa Viongozi wa serikali za mitaa kutoka wilaya za Nyamagana na
Ilemela mkoani Mwanza.
Semina
hiyo ya siku tatu, kuanzia jana Mei 09 imewashirikisha Madiwani,
Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, Wenyeviti wa
Mitaa na dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi imelenga kuwajengea
uwezo viongozi hao ili kusaidia kutetea na kulinda maslahi ya mtoto
mfanyakazi wa nyumbani na kumuepusha na utumikishwaji wa kazi ngumu na
maslahi duni.
Na BMG Habari
Mwanasheria
wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye
semina hiyo ambapo pia ameelezea juu ya umuhimu wa viongozi hao
kuitambua Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo
inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 14 kuajiriwa huku wale walio juu
ya umri huo wakipaswa kuajiriwa kufanya kazi zisizo hatarishi.
Aidha amekumbusha juu ya kuutambua Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 ambao unaelekeza
kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha
chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi
ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye
nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye
nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai
wakigeni.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia mada
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Semina hiyo ilianza jana Mei 09,2017 na inatamatika kesho Mei 11,2017 Jijini Mwanza
Afisa kutoka shirika la WOTESAWA akiwa kwenye semina hiyo
Diwani
wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, John Kabadi, amesema semina hiyo
itwasaidia katika kutetea maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani
ikiwemo kuwaepusha na utumikishwaji pamoja na ujira duni.
Gloria
Shindika kutoka dawati la jinsia, kituo cha polisi Igogo Jijini Mwanza,
amesema semina imewaongezea mbinu zaidi za namna ya kuwasaidia watoto
wafanyakazi wa nyumbani watakaokuwa wakikumbwa na aina yoyote ya
utumikishwaji.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Nyamanoro Kaskazini, Kata ya Ibungilo Manispaa ya Ilemela,
ameeleza kutumia elimu aliyoipata kwenye semina hiyo katika kuwaelimisha
wananchi wa mtaa wake katika kuhakikisha maslahi na haki za mtoto
yanalindwa
Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akizungumza na Lake Fm Mwanza
Shirika
la WOTESAWA linawahimiza wanajamii kwamba bado watoto wafanyakazi wa
nyumbani wanayo haki ya kupata elimu hivyo ni vyema haki hiyo
ikazingatiwa.
Tags
MAYAYA