Timu ya VIONGOZI wa serikali
chini ya uongozi wa kocha mchezaji Mkuu wa Mkoa wa Mbeya imeibamiza
bila huruma timu ya VIONGOZI wa DINI mabao 4-1
Mpira ulikuwa mkali ila timu ya VIONGOZI wa serikali iilionekana kucheza kwa maelewano hivyo kuisaidia timu hiyo kuibuka mshindi na kumaliza tambo za muda mrefu za timu hizo angalia matukio katika picha hapa chini
Mpira ulikuwa mkali ila timu ya VIONGOZI wa serikali iilionekana kucheza kwa maelewano hivyo kuisaidia timu hiyo kuibuka mshindi na kumaliza tambo za muda mrefu za timu hizo angalia matukio katika picha hapa chini
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos
Makalla akikokota mpira mbele ya mchezaji wa timu ya viongozi wa dini
katika mchezo uliofanyika leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku
viongozi Timu ya viongozi wa Serikali ikitoka kifua mbele kwa kushinda
magoli 4-1 dhidi ya timu ya viongozi wa dini.
Wachezaji wa timu za viongozi wa
Dini na Viongozi wa Serikali zikichuana vikali kwenye uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika leo.
Mchezaji wa timu ya Viongozi Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akinyanyua juu kombe waliloshinda
dhidi ya timu ya viongozi wa Dini katika mchezo wa mpira wa miguu
uliofanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine.
Mchezaji wa timu ya viongozi wa
serikali na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akizungumza na vyombo
vya habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kwye uwanja wa
Sokoine ambapo timu yake imeifunga timu ay viongozi wa dini magoli 4-1.
Wachezaji wa timu ya viongozi wa serikali wakipiga picha ya pamoja na kombe lao mara baada ya ushindi huo.
Timu ya viongozi wa dini
ikikaguliwa na mgeni rasmi kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliofanyika
kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Tags
VIONGOZI WA DINI