
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair ametangaza kuwa anarejea
tena kwenye siasa za Uingereza ili kupambana dhidi ya uamuzi wa
kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya, maarufu Brexit.
Blair ambaye alikiongoza Chama cha Labour kuanzia mwaka 1994 hadi 2007,
hata hivyo hatagombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni
8.
Lakini ataunda vuguvugu la kisiasa juu ya majadiliano ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya.
Blair (63), ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa muongo mmoja
kuanzia mwaka 1997, alisema anafahamu uamuzi wake huu utakumbwa na
ukosoaji mkali.
Lakini alisema si sawa kwake kuachia suala la Brexit liende kama liendavyo, bila kutoa mchango wake.