Mbuge wa Dodoma Mjini Dk. David Malole
ambae ni mjumbe wa Bodi ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), akionyeshwa
miti na mabaki mengine na Mtemi Lazaro Chihoma namna Makumbusho hayo ya
kimila yaliyojengwa katika mlima wa Bwibwi yalivyobomolewa na CDA.
Mjumbe wa Kamati ya siasa CCM Wilaya ya
Dodoma Judith Myeya akifafanua jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari mala baada ya kujionea jinsi makumbusho ya kimila ya kabila la
kigogo yalivyobomolewa na Mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA, na
kupendekeza mamlaka hiyo ifutwe.
Mtemi Lazaro Chihoma Akiwaonyesha baadhi
ya watu wakiwemo Mbunge wajimbo la Dodoma mjini Dk. David Malole na wa
CCM waliofika kuona jinsi makumbusho hayo ya kimila yalivyovunjwa na
CDA.
Chief Lazaro chihoma (katikati),
akiwaongoza Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Dk. David Malole, Katibu
Mwenezi wa CCM wilaya Salum Kalli, mjumbe wa ya siasa wa wilaya CCM,
Judith Myeya na viongozi wengine kuona sehemu ya Ikulu ya kimila
ilivyohalibiwa na CDA.
Wananchi wa kijiji cha Iyumbu wakiwa
wamejiinamia wasijue la kufanya baada ya tinga tinga la CDA kufika na
kubomoa Makumbusho ya kimila yaliyojengwa katika mlima wa Bwibwi chini
ya ulinzi mkali wa polisi mwishoni mwa wiki.
Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya
Usitawishaji Makao Makuu (CDA), Dk. David Malole akijadiliana jambo na
Mtemi wa kabila la Kigogo Lazaro Chihoma (kulia) na Mzenge Tumbi Andason
Chaulema kwenye makumbusho ya kimila yalibomolewa na Tinga tinga la CDA
chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Nyama za mbuzi na ngombe ni bidhaa pekee
inayochangamkiwa sana na wananchi wa ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma
wakiwemo Wabunge katika Mnada unaofanyika kila siku ya Jumamosi uliopo
Msalato, mkoani Dodoma. Wachomaji hawa walinaswa wakiwa kazini mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Mtemi wa Makumbusho ya Kimila, Lazaro
Chihoma akitoa tangazo la kuendelea na ujenzi kwa mara nyingine mbele ya
waandishi wa habari siku moja tangu makumbusho hayo, yaliyopo katika
Mlima wa Bwibwi kubomolewa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA),
mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Iyumbu
akiendelea na ujenzi wa moja ya nyumba za matambiko ya kimila kwa kabila
la kigogo siku moja baada ya CDA kufika na kubomoa nyumba hizo
zilizojengwa kwa miti juu na chini bila kujali kisima chenye kumbukumbu
za kihistoria kilichopo katika eneo hilo. (PICHA ZOTE NA JOHN BANDA WA BANDABLOG)