Uhamisho
wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United uliovunja
rekodi ya dunia sasa unachunguzwa na shirikisho la soka duniani Fifa.
Fifa imeandika barua kwa klabu hiyo ya ligi ya Uingereza ikitaka maelezo zaidi.
Shirikisho hilo linataka kujua ni
nani alyeshirikishwa katika uhamisho huo wa kitita cha pauni milioni
89.3 na ni fedha ngapi zilizolipwa.
Msemaji
wa klabu ya Manchester United :Hatuzungumzii kuhusu kandarasi za watu
binafsi.Fifa imekuwa na nakala hizo tangu uhamisho huo ufanyike mwezi
Agosti.
Pogba anahudumia msimu wake wa
pili katika uwanja wa Old Trafford, baada ya kuondoka katika klaabu hiyo
na kuelekea Juventus kwa kitita cha pauni milioni 1.5 mwaka 2012.
Raia huyo wa Ufaransa mara ya kwanza alijiunga na United kutoka klabu ya Ufaransa ya Le Havre 2009 kwa hali ya utata.
Alirudi katika klabu hiyo msimu uliopita kwa kitita kilichovunja rekodi cha Yuro milioni 105.
United pia ilikubali kuilipa
Juventus Yuro milioni 5 kwa malipo ya ziada pamoja na gharama nyengine
iwapo Pogba atatia saini kandarasi mpya.
Wakati walipothibitisha uhamisho
huo, Juventus ilisema kuwa uhamisho huo umeimarisha uchumi wa klabu hiyo
na kufikia Yuro milioni 72.6
Tags
MICHEZO KITAIFA