
Wazazi poleni kwa msiba huu uliowapata watoto wetu wapendwa wa Lucky
Vicent na walimu wao! Hakika ni majonzi makubwa sana! Lakini yafaa
tutafakari kwa kina kwanini janga kama hili liwafike watoto hawa,
tumaini la maisha yetu! Maswali ni mengi, na kwa kweli yana hitaji
majibu ya kina.
Kwa tunaozunguka kutwa barabarani, mtakubaliana na mimi kuwa, vipo
viashiria vingi hatarishi kwa watoto wetu wanapotumia mabasi ya shule
zao. Shule nyingi zinatumia mabasi ambayo zamani yalitumika kama
daladala, na baada ya kuchoka yakabadilishwa na kuwa mabasi ya shule.
Huku madereva wakiendesha kwa mwendo usiostahili kabisa kubeba watoto.
Hatari zaidi, mabasi haya ya shule hubeba idadi kubwa ya wanafunzi
kuzidi uwezo halisi wa gari, na kutokuzingatia taratibu zote za
kiusalama kama vile kufunga mikanda. Mfano wa hili ni hii ajari ya Lucky
Vicent. Wanasema "eti gari lili feli breki" ndo sababu ya ajari!
Binafsi sikubaliani nalo.
Kwa wale ambao wameendesha magari makubwa kwa weledi na kwa kipindi
kirefu, watakubaliana na mimi kuwa, kubeba uzito zaidi ya uwezo wa gari
pamoja na mwendo kasi husababisha mfumo wa breki za gari kushidwa
kuhimili, hivyo kutokukamata pale dereva anapozitumia.
Sababu nyingine ya kujiuliza, je ni kweli haya mabasi ya shule
yanafanyiwa matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara, kwa maana ya motor
vehicle service! Hapa inatiashaka! *A motor vehicle service is a series
of maintenance procedures carried out at a set time interval or after
the vehicle has travelled a certain distance.* Shule ya Lucky Vicent
lazima ithibitishe kwa kuonyesha *service na log books* za hilo gari,
majibu utayaona, hakuna kumbukumbu ya service.*The completed services
are usually recorded in a service book which is rubber stamped by the
service centre upon completion of each service.* Mashule mengi yanahuo
udhaifu, na hii inatokana na uzembe, tamaa, ubadhirifu wa watendaji wao,
kutokujali maisha ya wanafunzi na kutokuwa waangalifu huku wakiweka
mbele masilahi yao na kupata faida.
Matengenezo muhimu na ya mara kwa mara kwa gari *motor vehicle service* ni kama ifuatavyo;
-Change the engine oil & oil filter
-Replace the air filter & fuel filter
-Tune the engine
-Check level & refill brake fluid/clutch fluid
-Check Brake Pads/Liners, Brake Discs/Drums, and replace if worn out.
-Check level and refill power steering fluid
-Refill Manual Transmission Fluid,Grease and lubricate components inspect.
-Check condition of the tires
-Check for proper operation of all lights, wipers etc.
Vipuri vingine vyote vinavyo weza kulifanya gari lisiwe salama kwa
matumizi ya barabara hukaguliwa na kubadilishwa wakati wa kufany
*service* je mashule yetu wanafanya haya! Kama haya hayafanyiki ni
wakati sasa wazazi wa watu wote wenye matashi mema kuchukua hatua za
kuwawajibisha wahusika wote ili kuokoa maisha ya watoto wasio na hatia.
Tags
Ajali ya Basi