
Hatua aliyoichukua Rais juu ya swala hili la Mchanga wa dhahabu ni
kitendo kilichoonesha umakini na nia ya dhati ya serikali kusimamia
rasilimali zetu hivyo kuongeza imani waliyokuwa nayo wananchi juu ya
awamu hii ya uongozi.
Wakati hilo likitokea kitendo hicho cha rais ni moja ya misumari muhimu itakayosiliba kabisa matumaini ya wapinzani.
Kauli za baadhi ya wapinzani katika kukosoa kitendo hiki cha kizalendo
ni matokeo na hasira za kupunguziwa hoja za kuinenea mabaya serikali.
Ni jambo lililowazi kuwa mambo hayakuwa sawa huko migodini wengi
walilalamika hilo limedhihirishwa na matokeo ya kamati ya wataalam
aliyoiunda Rais.
Ila baada ya juhudi hizo za wazi kuonesha mwanga wa utatuzi wa
malalamiko yetu ya muda mrefu; wale wale waliokuwa kati ya walalamishi
wameanza kugeuka kauli zao na kuanza kutuambia kwamba kilichofanyika ni
makosa eti tutapata hasara kama Taifa.
Kauli hizo na nyingine nyingi toka upinzani zinatufanya baadhi yetu
tuanze kujiuliza lengo halisi la upinzani hapa nchini ni nini?
Je malengo ya upinzani ni kuibua mabaya tu ili kupata umaarufu?
Je; serikali inatakiwa kukosea tu kila mara ili ikosolewe na upinzani?
Je; serikali haina haki ya kufanya mambo sahihi kwa watu wake?
Je; ni upinzani pekee ndio wenye haki ya kufanya mambo sahihi kwa wananchi.
Je; ni lazima upinzani ukosoe hata yale mazuri ya serikali?
Mwisho wa yote fikra zinamuongoza mtu kuona kama jambo hili jema
limepunguza kete za upinzani na upinzani hawajalifurahia kwakua wanakosa
agenda za kwenda nazo kwa wananchi.
Na fikra hizo hizo zinakutuma kuona kwamba upinzani wamekosa uzalendo na zaidi sana wanawaza umaarufu wao.
Tags
mchanga wa madini