
Kama mlivyosikia kwamba ukiwa na vyerehani vinne tayari ni kiwanda, yaani ukiwa na vyerehani 40 una viwanda 10.
Hii issue imenikumbusha mwaka 2013, kuna rafiki yangu flani alikua
anafanya kazi kwenye kampuni flani ya wahindi ina deal na security,
firefighting na mambo ya cartrucking, sasa wao walikua kitengo cha
Marketing na mhindi flani, wanachofanya wanaenda site kuongea na wateja
ambao sometimes wanawapata kupitia majarida mbalimbali na kuwapigia
simu.
Sasa bwana wakaongea na Mangi mmoja kwenye simu kwamba wao wanatoa
huduma mbalimbali kwenye makampuni, maduka, na office mbali mbali, basi
wakapanga appointment, kumbuka kazi wanazofanya wao ni kwenye office
kubwa kubwa, kwenye makampuni makubwa.
Sasa siku ya siku ikafika asubuhi na mapema wakaingia kwenye "NAVARA"
safari ya kwenda kwa Mangi kibaha maili moja ikaanza, kichwani
wanaimagine huko tutakuta supermarket, au kiwanda flan, au jamaa atakua
ni Transporter, basi bwana, gia mosi, gia pili mara kibaha mizani ya
zamani hii hapa, wakampigia simu, ndio tunaingia maili moja hapa tupe
ramani vizuri.. Mangi akawaelekeza.
Mara Vuuu, break zinakanyangwa mbele ya Mangi, walichokiona ilibidi
muhindi awashe sigara yake ya Malboro kwanza, ilikua ni kituko!! Yaani
walikuta ni kioski, yaani ni kiduka cha mbao kidogo dogo flan hivi
kimechoka sana, yaani kwa haraka haraka mali iliyokuwemo mule kioskini
ilikua kama ya laki mbili hivi au pungufu ya hapo, Jamaa hata hawakutaka
kuongea nae, wakatia reverse gear, wakarudi kinondoni wakiwa hoiii..
Sasa ukikumbuka jinsi CCM kupitia JPM ilivyokua inajitapa kuhusu viwanda
utacheka sana jinsi saivi wanavyoongelea hivi viwanda. Nakumbuka katika
mkutano wa kampeni uliofanyika kibaha JPM akiongozwa na Bulembo
waliongea maneno matamu sana kuhusu viwanda, ila kumbe walikua
wanamaanisha viwanda kama vyerehani na kijiwe cha "shoe shine" cha
kushonea viatu.
Na ili kulielewa hili wazia juzi wametangaza kua eti kiwanda cha
"General Tyre" kimetengewa milion 70 kukifufua, REALY??? Yaani kiwanda
cha matairi ukifufue kwa only 70,000,000? Pesa ambayo ambayo ukililia
sana ndo utapata horse ya scania mtumba flan hivi umechokachoka wa
R420!!
Yaani hiyo 70mil hakuna kitu itafanya, ikumbukwe hapo inainclude
material and operational cost... Ifike mahala serikali iache utani na
Nchi yetu. Wao wanatembelea chuma zenye thamani ya 200mil+ ila hata
kusema basi hiki kiwanda tukipe japo pesa yenye thamani ya VX V8 japo 5
tu hawawezi.
Ukweli ni kwamba mpaka miaka Mitano itakapoisha hakuna kiwanda chochote
kitakachosimama na kuwaajili Watanzania, hata hiyo General Tyre haiwezi
kusimama kwa 70mil..
Nchi ya viwanda na uchumi wa kati ilikua ni AHADI HEWA NA HADAA KWA UMMA
WA WATANZANIA. Sisi tumejizoelea maisha yetu ya kawaida tu, hamkua na
haja ya kututamanisha vitu msivyoweza kutimiza, leo unasema vyerehani
vinne ni kiwanda, basi sawa, kwahiyo basi hata kwa wakaanga chips ni
"Food Processing Industries"
Nimalize na mfano Huu; kuna siku rafiki yangu mwengine mbali na yule wa
hapo juu alijikoki na wenzie( kutoka Madrasa flani hivi Mabibo pale),
walikua wanaenda kufanya Dua/ kisomo kwenye nyumba flani hivi ya
Muarabu, kwenye akili yao wakajua leo huko kutakua na msosi wa nguvu
kuanzia Biriani na mazagazaga ya kutosha(si unajua tena hawa ndugu zetu
kwa msosi-samahani lakini, ni utani), maskini wakabeba ndizi wakazitia
ndani ya kanzu kila mtu kwaajili ya makamuzi, kufika pale hamna harufu
yeyote kusema labda msosi unasababishwa, wakajipa moyo anyway labda
muarabu kaamua kuagiza "catering" so after duaa mzigo utaletwa hapa,
weeeeeee, watu wamemaliza dua zimeletwa chupa za chai na biscuts..
Chanzo - Jf
Tags
VIWANDA