Habari/ Picha na Philemon Solomon.
……………………
Usiri
ni moja ya changamoto kubwa katika kushughulikia kesi za waathirika wa
ukimwi walioambukiza kwa makusudi tangu sheria ya kudhibiti watu
wanaoambukiza ukimwi kwa makusudi mwaka 2008 nchini.
Mkuu wa kitengo cha sheria kutoka Tume ya kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS), Elizabeth Kaganda.
Akizungumza mjini Dodoma wakati wa
semina ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na kamati ya kudumu ya
bunge ya kudhibiti Ukimwi iliyokuwa ikijadili utekelezaji wa sheria ya
ukimwi na haki za Binadamu, mkuu wa kitengo cha sheria kutoka Tume ya
kudhibiti ukimwi nchini (TACAIDS), Elizabeth Kaganda amesema kwamba
kifungu cha 47, cha sheria ya ukimwi namba 28 ya mwaka 2008, kwamba mtu
aliyeambukizwa ukimwi kwa makusudi anapaswa kutoa ushahidi na
ushirikiano kwa Jamhuri ili kuweza kufanikisha kesi hizo.
” tatizo linakuwa baada ya wale
walioambukizwa kuwa ni watu wazima na hawapo tayari kutoa siri ya
matatizo yaliyowakuta ( right to privacy) usiri ndio changamoto kubwa
kwa watu wazima kwa kuwa wengi hawapo tayari kuweka mambo yao ya siri
hadharani ” amesema kaganda,
Mbunge wa Kigamboni, Dk
Faustine Ndugulile ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya
masuala ya Ukimwi akizungumza wakati wa semina.
Pia Wabunge wa kamati ya kudumu ya
ukimwi wameitaka serikali kuja na uchambuzi wa sheria ya maambukizi
ukimwi, akizungumza na waandishi wa habari , Mbunge wa kigamboni, dk
faustine ndugulile amesema kwamba wabunge wanataka kujua kupitia sheria
ya kudhibiti ukimwi ni watu wangapi wametiwa hatiani kwa kosa la
kuambukiza wenzao kwa makusudi.
Alisisitiza kwamba pia wabunge
wameonyesha wasiwasi kwa sababu unapopima mtu afya yake ni siri yake
kwahiyo ni ngumu kumuweka hadharani lakini hapo wana jukumu LA kulinda
jamii.
Amesema wabunge walikuwa kwenye
semina kupitia kamati yao ya ukimwi na madawa ya kulevya katika juhudi
za kuendelea kupambana na janga hilo katika jamii.
Kuna udhaifu Mkubwa katika sheria ya kuzuia maambukizi ya ukimwi ya makusudi.
Naibu waziri wa kazi, ajira, vijana na walemavu, Anthony Mavunde.
Naibu waziri wa kazi, ajira,
vijana na walemavu, Anthony Mavunde amesema kwamba serikali itakwenda
kubadilisha sheria ili kupunguza udhaifu na mapungufu katika kuendelea
kuzuia maambukizi ya ukimwi kwa makusudi ndani ya jamii.
“serikali imepokea maoni ya
wabunge juu ya mapungufu ya sheria ya maambukizo ya ukimwi kwa makusudi
na inakwenda kuifanya kazi ili kuendelea kuilinda jamii kwa kuiangalia
upya hayo mapungufu, ” amesema mavunde
Kamati ya kudumu ya bunge ya
ukimwi na madawa ya kulevya na wahariri wa vyombo vya habari watakaa
pamoja ili kujadili hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini
pamoja na sheria ya mwaka 2008 na changamoto zake
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Tacaids, Yasin Abbas akitoa mada.
Wabunge wakichangia mada mbalimbali wakati wa semina
ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na kamati ya kudumu ya bunge ya
kudibiti Ukimwi iliyokuwa ikijadili utekelezaji wa sheria ya ukimwi na
haki za Binadamu.
Wabunge wakichangia mada mbalimbali wakati wa semina
ya wahariri wa vyombo vya habari pamoja na kamati ya kudumu ya bunge ya
kudibiti Ukimwi iliyokuwa ikijadili utekelezaji wa sheria ya ukimwi na
haki za Binadamu.
Tags
UKIMWI