Bw. Boniface Myala akizungumza
na wanafunzi alipotembelea shule ya Msingi Kunguru Goba na kugawa
madaftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza leo jijini Dar es
Salaam.
Bw. Boniface Myala akikabidhi
daftari kwa Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani leo jijini Dar
es Salaam.(Na Mpiga pich Wetu)
Bw. Boniface Myala akigawa
daftari kwa wanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Kunguru
Goba . Leo jijini Dar es Salaam.
………………………………
Watanzania wametakiwa
kuisaidia serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ili
kujiletea maendeleo kwa haraka badala ya kusubiri kila jambo lifanywe
na serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Mdau
wa Maendeleo Bw. Boniface Myalla wakati alipotembelea shule ya Msingi
Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la
kwanza.
Mayala amesema, Watanzania
hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali inayoongozwa
na Rais Dk.John Pombe Magufuli za kuhakikisha inaleta maendeleo na
huduma bora kwa wananchi.
“Serikali imetekeleza jukumu
lake la kutoa elimu bure, imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya wanafunzi
kusoma bure, sasa imebaki upande wetu wazazi na walezi kuwawezesha
wanafunzi kupata vifaasaidizi,” amesema.
Amesema lengo la kutoa
madaftari hayo ni kuunga mkono serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli
katika dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengeka, Tanzania
ambayo kila Mtanzania atanufaika na nchi yake lakini pia kupata elimu
bora.
Akizungumza baada ya kupokea
zawadi hizo, Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani amemshukuru
Myala na kuiomba serikali na wadau wengine kujitokeza na kutoa msaada
ili kukamilisha malebgo na ndoto za wanafunzi.
Amesema wapo wanafunzi
walikjuwa wakishindwa kuandika kwa kukosa madaftari na vifaa vingine vya
kujifunzia hivyo ujio wa madaftari hayo utapunguza kero changamoto
hiyo.
Tags
ELIMU