
Chama cha ACT-Wazalendo kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kikieleza kuwa amevunja mwiko wa
siasa za Tanzania baada ya kufanya teuzi kutoka katika vyama pinzani ili
kuwaletea wananchi maendeleo.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Samsoni Mwigamba
wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
amesema kuwa kwa hatua hiyo aliyoonyesha Rais Magufuli, sasa ni wakati
wa watanzania kuanza kuona kuwa taifa hili ni letu sote.
Aidha, Mwigamba amesema kuwa chama chao hakioni tatizo lolote kwa uteuzi
wa aliyekuwa mwenyekiti wao, Anna Mghwira ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, huku akisisitiza kuwa ni jambo jema kwani
ameteuliwa ili akawaatumikie wananchi. Tazama hapa
Tags
ACT- Wazalendo