
Hali ya sintofahamu imekikumba chama cha ACT-Wazalendo baada ya
Mwenyekiti wa chama hicho kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt.
John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Hayo yametokea mara baada ya Afisa Habari wa chama hicho, Abbdallah
Khamis kushindwa kuelezea undani wa tukio hilo huku ikisemekana baadhi
ya wanachama kutoa shinikizo la kukataa uteuzi huo alioteuliwa na Rais.
“Uteuzi huo hata sisi tumeusikia kwenye vyombo vya habari, hivyo chama
kitakaa kikao na Mwenyekiti wetu ili tuweze kuzungumza nae, kani kwasasa
siwezi kuzungumzia chochote kwasababu muhusika yupo safarini, hata
Zitto naye kasikia kwenye vyombo vya habari hivyo baada ya kikao chama
kitatoa tamko,”amesema
Tags
ACT- Wazalendo