KIONGOZI wa mbio za
mwenge kitaifa 2017 ,akielezwa namna kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya
Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited
kilichopo Kibaha Mkoani Pwani,kinavyozalisha bidhaa zake ,wa tatu kulia
,kaimu meneja masoko ,Frank Mzindakaya .
Kaimu
mkurugenzi kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa
Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited kilichopo Kibaha Mkoani
Pwani,Samwel Mziray akimkabidhi kiongozi wa mbio za mwenge taarifa ya
kiwanda hicho .(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WANANCHI na
halmashauri nchini zimetakiwa kununua bidhaa zinazozalishwa Tanzania
ikiwemo dawa za kuua viluwiluwi vya mbu wa malaria zinazotengenezwa
Kibaha ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Amesema ni wakati wa
watanzania kuwa wazalendo wa kupenda vyao kwani Tanzania ya viwanda ni
kuangalia masoko ya bidhaa za ndani na kupiga vita vinavyozalishwa nje .
Kauli hiyo ilitolewa
na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2017 ,Amor Hamad Amor wakati
alipokwenda kuzindua kampeni ya kudhibiti malaria Kibaha Mji na
kutembelea kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu
wa Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited .
Alisema, dawa za kuua
viluwiluwi vya mbu wa malaria zinapaswa kununuliwa na kila halmashauri
kutoka kiwanda hicho kinachomilikiwa na serikali kwa asilimia 100.
Hata hivyo ,Amor alieleza mpaka sasa mwitikio wa jamii na halmashauri hauridhishi .
“Tunajirejesha nyuma
kimasoko lakini mkumbuke lengo la Serikali ni kupunguza vifo vitokanavyo
na malaria nchini hasa kwa akinamama wajawazito na watoto chini ya
miaka mitano”, alisema Amor.
Alisema kwamba iwapo
kama halmashauri hasa zilizopo Bara zitanunua dawa hizo na kuzitumia,
ugonjwa huo utapungua kwa kiasi kikubwa na kuwa kama Zanzibar ambayo
ugonjwa huo upo kwa asilimia moja.
Amor alielezea kuwa,
kazi ya kupambana na malaria ni ya kila mmoja hivyo tupambane kwa
kununua dawa hizo pasipo kujirudisha nyuma kimasoko .
Alimpongeza Rais wa
awamu ya nne ,dk.Jakaya Kikwete kwa kuwa chanzo cha kuwepo kiwanda hicho
kwa lengo la kuhakikisha kwamba Tanzania inakua huru dhidi ya malaria .
” Niwahakikishie
kuanzia sasa nitakuwa balozi wa kutangaza kiwanda na dawa hizo kwa kila
halmashauri atakayopita ili kutoa msukumo wa kununulika bidhaa hiyo.
Nae kaimu meneja mkuu
wa Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa
Malaria cha Tanzania Biotech Products Limited, Samwel
Mziray alisema,kwa sasa wanazalisha dawa za aina mbili ambazo ni
Bactivec na Griselesf zinazotumika kwa kunyunyuzia katika mazalia ya
mbu.
Alifafanua pia
wanazalisha kwa wingi dawa hizo ambapo alitaja moja ya nchi iliyonunua
dawa hizo ni Niger ambayo tayari imenunua zaidi ya lita 91,000 na nchi
nyingine za Serbia na Srilanka ziko katika mazungumzo ya kununua dawa
hizo.
“Nikuombe kiongozi wa
mbio za mwenge kitaifa,kutoa ujumbe wa kutangaza dawa hiyo kwa
halmashauri ambazo bado hazijanunua dawa hizi kukitumia kiwanda hiki
kufikia malengo ya Rais dk ,John Magufuli”, alisema Mziray.
Mziray alisema kwa wiki wanazalisha lita 42,000 na zina uwezo mkubwa wa kuangamiza viluwiluwi vya mbu wa malaria.
Kuhusu agizo la
Serikali la kuzitaka halmashauri nchini kununua dawa hizo tayari
utekelezaji huo umefanywa na wilaya ya Kibaha kupitia ofisi ya mganga
mkuu Mkoa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji kwa kufanya majaribio
kwenye kata mbili za Mkuza na Visiga na wamejiridhisha .
Kaimu meneja masoko
na mauzo kiwandani hapo, Frank Mzindakaya alieleza, serikali inapaswa
kutenga bajeti ya kutosha ili kuziwezesha halmashauri kununua dawa hizo.
Alisema, dawa za kiwanda hicho wanaziweka katika vipimo mbalimbali ikiwemo vya lita 20 na ujazo wa miligramu 30 .
Mziray aliwaomba dawa
hiyo itumike kwani ikimwagwa katika madimbwi makubwa huua mbu wrote na
hatimae kuwalinda wananchi dhidi ya malaria”, alisema Mzindakaya.
Akielezea juu ya
kiwanda hicho ,Mzindakaya alifafanua ,kuwa Tanzania Biotech Products
Limited ni Kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo (NDC) iliyopewa
dhamana ya kusimamia na kuendesha kiwanda cha kuzalisha bidhaa hizo.
June 6 mwaka
huu,mwenge wa Uhuru umepokelewa wilayani Kibaha ,kutoka Kisarawe
,ambapo ukiwa Kibaha ulitembelea miradi 10 yenye thamani ya sh .bilioni
13.775.965 .
Awali
akikabidhi mwenge huo ,mkuu wa wilaya ya Kisarawe ,Happiness Seneda
,alisema June 5 ,mwenge wa Uhuru ,ulitembelea miradi saba iliyogharimu
bilioni 3.1 .
Tags
malaria