Mashauri 18 ya madai ya kodi ya ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 yamewasilishwa katika
Baraza la ardhi na nyumba wilaya ya Tanga ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuwabana wamiliki wa viwanja wanao kwepa kulipa kodi.
Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa mashuari hayo mwakilishi wa afisa ardhi msaidizi kanda ya kazikazini Thadeus Riziki amesema hatua ya kuwafikisha mahakamani wamiliki wa viwanja hivyo ni kupata kibali kitakacho wezesha wizara kulipwa makusanyo ya madeni
Amesema baada ya halmashauri kuwapelekea wamiliki hati ya madai na kushindwa kulipa hatua inayofuata ni kuwafikisha mahakamani ili kupata ridhaa ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa.
Kwa upande wake afisa ardhi mteule Halmashauri ya jiji la Tanga Straton Thobias amesema katika mwaka wa
fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3
Akizungumzia zoezi hilo mwanasheria ofisi ya kamishina wa ardhi Rosemery Mshana amesema wamiliki wa ardhi
wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani mujibu wa kifungu cha 50 cha sheria ardhi namba nne(4)
habari kwa hisani ya blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Tags
UKWEPAJI KODI