Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde akiteta
jambo na Sheikh wa Mkoa huo, Mustafa Shaban Rajab katika baraza la Eid
El Fitr lililofanyika Uwanja wa jamhuri mjini Dodoma.
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Baraza la Eid kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde
akisikiliza kwa makini mawaidha katika Baraza la Eid.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde
akisikiliza kwa makini mawaidha katika Baraza la Eid.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde
akisikiliza kwa makini mawaidha katika Baraza la Eid.
………………………………………………………………………..
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde
amewaomba waumini wa dini ya kiislamu na watanzania kumuombea Rais
Dk.John Magufuli ili Mwenyezi Mungu amjaze Ujasiri, Hekima na Maarifa.
Akizungumza leo katika Baraza La
Eid el fitr Mkoa wa Dodoma lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri
Dodoma lililoongozwa na Sheikh wa Mkoa huo, Mustafa Shaban Rajab,
Mavunde amesema ni vyema watanzania na waumini hao kumuombea Rais kwa
kuwa anadhamira ya kweli ya kuwatumikia watanzania.
Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Dodoma mjini, amesema maombi zaidi yanahitajika hasa katika
kipindi hichi cha kupambana rushwa, ufisadi na vita dhidi ya Uhujumu
uchumi.
“Waislamu na watanzania kwa
ujumla wenye mapenzi mema na Taifa hili ni vyema mkamuombea Rais wetu
ili aendelee kuliongoza Taifa Tanzania na kupambana na vitendo viovu
vinavyorudisha nyuma Taifa kimaendeleo,”amesema Mavunde
Aidha ametumia nafasi hiyo
kuwatakia Waislamu wote heri ya sikukuu ya Eid na kuwaomba viongozi wa
Dini kuendelea kuhubiri kuhusu Upendo, Umoja na Mshikamano miongoni mwa
watanzania bila kujali tofauti ya itikadi za vyama,dini, rangi wala
kabila.
Tags
BARAZA LA EID