
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na
kusema suala la kuongoza nchi ni kazi kubwa mno na kusema yeye toka
amestaafu kazi hiyo saizi anaweza kulala na usingizi ukaisha vizuri
lakini kipindi cha nyuma haikuwa hivyo.
Kikwete amesema hayo jana kwenye Futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni
ya simu za mkononi nyumbani kwake Msoga, Pwani na kusema saizi mzigo
huo ameubeba Rais Magufuli na kudai huwa anamtia moyo kuwa anapaswa
kupambana kwani hata wao wamepitia mambo ambayo yeye anapitia.
"Sasa nimestaafu muda wa kuwasaidieni ninao tofauti na zamani, zamani
mambo mengi kubeba mzigo wa kuongoza nchi kazi kubwa sana saizi
anahangaika nao Rais Magufuli wakati mwingine nampa moyo tu bwana wewe
pambana, wenzako wote ndiyo hivyo hivyo tulipitia humo humo pale
unapodhani unatenda jema asubuhi wanakuponda, ndiyo muziki wenyewe
lakini mara kuna hili kuna lile saizi mimi nalala usingizi unaisha
kabisa kama kuna watu wananisumbua watakuwa ni wajukuu tu" alisema
Kikwete