ABDUL DUNIA
Titi la Mama ni tamu. Hata likiwa
la mbwa. Kiswahili naazimu. Sifayo inayofumbwa. Niimbe ilivyo kubwa.
Toka kama chemuchemu.Titi la Mama litamu jingine haliishi hamu. Aliwahi
kuandika hayati Shaban Robert katika moja ya vitabu vyake.
Nimemaliza kufuturu hapa kwa mama
Dunia. Futari yake imenikumbusha mbali sana. Tangu mwezi uanze hii ndiyo
futari yangu ya kwanza kwa mama yangu. Futari yake imenikumbusha hayo
maneno magumu ya nguli huyo. Shaban Robert ni kati ya waandishi
walitokea kunivutia kutokana na kalamu yake anapoitumia. Hakuna kama
Shaban Robert. Acha niishie kusema hivyo.
Baada ya kushiba futari nimekaa na
zile kaseti mbili za Azam TV. Moja kwenye mechi kati ya Simba na Mbeya
City. Nyingine Yanga na Ruvu Shooting. Zote za msimu uliopita.
Nimetazama kaseti hizo na
nimezielewa. Nimeona wachezaji wawili tu. Kwanza nimemuona Ibrahim Ajab
alafu nimemalizia kumuona Haruna Niyonzima maarufu kama Fabregas. Hao tu
ndio niliowaona katika mechi hizo.
Kufananishwa na mtukama Fabregas
sio jambo dogo kabisa. Lazima uwe na kitu cha ziada ile kweli
ufananishwe naye. Si mlimuona yule Idrisa maarufu kama Ronaldo wa Misosi
Fc. Kapiga tano pekee yake. Hakika anafaa kuitwa Ronaldo.
Nimemuona Ajibu akifunga bao la
kusawazisha kwa faulo ya moja kwa moja. Kisha nimemuona Niyonzima
akiimaliza Ruvu Shooting kwa pasi yake murua iliyomfanya mmoja wa mabeki
kuanguka kama mzigo wa karanga. Mwisho nimemuona Niyonzima akimvisha
kanzu beki. Ghafla nikaikumbuka ile kanzu ya Zinedine Zidane dhidi ya
Ronaldo De Lima mwaka 1998.
Kuna vitu wanavyojaribu kuvifanya
wachezaji hawa, sio vya kwenye Ligi yetu kabisa. Hakika tumewahi
kuwashuhudia watu wakila kanzu miaka ya nyuma sana. Zama za kina Method
Mogela na Athuman Chama ndio kipindi cha watu walipokuwa wakipigwa kanzu
sio kipindi hiki cha sasa. Tuachane na hilo.
Mwishoni mwa wiki hii kuna taarifa
zilizoenea kuwa Ajibu amesaini Yanga. Leo kuna mtu ameniambia kuwa
Niyonzima amesaini Simba. What a football?
Huu ndio mpira wa kweli. Niyonzima
Simba alafu Ajib Yanga. Ni nadra sana katika Ligi moja wachezaji muhimu
kuondoka ndani ya msimu mmoja huku wakibadilishana timu. Hakika ni mara
chache sana kwa tukio kama hili.
Katika moja ya maandiko ya mzee
Arsenal Wenger aliwahi kusema kuwa ‘Footballer is Most Hypocrite people
in the world” akiwa na maana kuwa wachezaji ni moja kati ya watu
wanafiki duniani. Tuliamini kama moyo wa Niyonzima utapokea kelele za
mashabiki wa Simba? Akili ya Ajibu itakubali lawama za Simba? Kila kitu
acha kimalizike lakini mpira uwepo kwanza.
Hapo awali mashabiki wa Simba
wa.limzomea Niyonzima. Yanga wakamzomea Ajib. Lakini leo. Kila mmoja
anakaribisha wa kwake. This is Football and Football is Fair Play Game.
Naanza kuiamini FIFA ilipotueleza hilo.
Kama Torres alikubali kutoka
Liverpool kwenda Chelsea. Raul Meireles pia. Ajib anaachaje. Niyonzima
anaachaje? Huu ndio unafiki aliouzungumzia Wenger. Ronaldo anamapenzi na
United lakini alikwenda Real Madrid. Huwezi kuzuia pesa kwa moyo wa
mapenzi. Steven Gerard hadi leo bado anajaribu kujifariji kwa dhambi
aliyoifanya mwaka 2005.
Gerard kwenye ubora wake.
Liverpool inatwaa UEFA pale Instanbul. Real Madrid, Barcelona na FC
Bayern Munich zinamtaka. Alichokifanya ni kuweka mapenzi na Liverpool.
Akapoteza alichoandikiwa kukipata. Anyway tuje kwenye mada muhimu.
Ajibu anakwenda kuikosa akili ya
Niyonzima. Niyonzima anakwenda kuikosa miguu ya Ajibu. Najaribu
kufikiria kama wawili hawa wangekuwa kwenye timu moja. Hakika hakuna
zaidi ya kupigiwa mpira mwingi. Hakuna zaidi ya hicho.
Hebu jaribu kufikiria zile Auta za
Ajib na Chenga za Niyonzima. Umakini wa Ajib na pasi za Niyonzima.
Mizuungusho ya Ajib na ufundi wa Niyonzima. Ukiwa na watu hawa kwenye
timu humuitaji tena Ngoma wale Tambwe. Chirwa mmoja anakutosha.
Kuwa na watu kama Niyonzima na Ajibu kwenye timu moja. Huitaji uwepo wa Mavugo wala Blagnon. Waziri Junior ama John Bocco tu wanakutosha. Hakika wanakutosha.
Jaribu kufikiria zile chenga za
Ajibu na kanzu za Niyonzima na ule utimamu wa Chirwa wakiwa kwenye timu
moja. Najaribu kuufikiria uwezo wa ‘Mo’ Mohammed Ibrahim, Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajib wakiwa kwenye timu moja. Hakika niliwahi kuomba itokee hii lakini imekuwa ngumu kidogo.
Unaachaje kujisifu unapokuwa na
Ajib na Niyonzima kwenye timu yako. Uwepo wa Ajib na Niyonzima ni sawa
na ule uwepo wa Zidane na Ronaldo pale Real Madrid. Chenga utapigwa na
kufungwa utafungwa tu. Hakika this is football.
Watu hawa wamekosana. Vipaji vyao
vimekosana. Uwepo wao pia umekosana. Katika vitu ambavyo nafikiria Ajib
na Niyonzima walitakiwa kuviomba nikuwa kwenye timu moja. Lakini imekuwa
ngumu kwao.
Acha nizirudishe hizi kaseti
kwenye kabati maana machozi yameshaanza kunilenga. Napomuangalia Ajib
alafu Niyonzima naona ule uwepo wa Christiano Ronaldo na Wayne Rooney.
Manchester United ikitwaa UEFA dhidi ya Chelsea.
Tags
usajili wa wachezaji