
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwingulu L. Nchemba, amekabidhi gari la
kubebea wagonjwa ambalo limetolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Jinsia, Wazee na Watoto kwa kituo cha afya cha Ndago kilichopo Wilayani
Iramba.
Aidha, amesema kuwa ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya
ambulance hiyo au gharama yoyote ile na kuwataka wagonjwa kutumia gari
hilo bure bila kuchajiwa gharama yeyote.
“Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote, liwe na mafuta ya kutosha na
dereva awepo. Gari hili ambalo ni la kisasa litunzwe na kulindwa ili
liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo”, amesema Mwigulu.
Hata hivyo, Mwigulu ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya rais
Magufuli na waziri Ummy kwa msaada huo ambao utaokoa wapiga kura wake na
wananchi kwa ujumla.
Tags
Mwigulu Nchemba