
Nguli wa soka, David Beckham ambaye hivi karibuni alikuwa nchini
Tanzania, amezua mjadala wa kimalezi baada ya kuweka mtandaoni picha
inayomuonesha akimpa busu zito la mdomo mwanae wa kike.
Baadhi ya wazazi walielezea picha hiyo kuwa haikuwa na maadili na
inashangaza kwa kuzingatia kuwa mwanae Harper ana umri wa miaka mitano
tu.
“Kwa kuwa mkweli, kumbusu mwanao wa kike mdomoni kama hivi kidogo inashangaza… ndio inashangaza,” aliandika mtu mmoja.
“Ninajaribu kutohukumu lakini nashindwa, lakini nadhani kidogo
inashangaza na sio sawa kuona anambusu mwanae kwenye midomo kwa
kuzingatia umri wake,” aliandika mwingine.
Hata hivyo, wazazi wenye mtazamo tofauti walijitokeza kumtetea mwanasoka huyo ambaye ni baba wa watoto wanne.
“Ni picha nzuri ya upendo inayoonesha uhusiano mzuri kati yako (Beckham) na binti yako,”
aliandika shabiki mmoja. “Achana na wenye chuki. Ni wapumbavu. Harper
sio binti mdogo, ni mtoto mdogo tu na hakuna ubaya kwa hilo,” aliandika
mwingine.
Hivi karibuni, Beckham alionekana akiingia Tanzania kwa ajili ya
kutembelea mbuga za wanyama, akiwa na familia yake. Ujio huo ulionekana
kuwa binafsi na wa kimyakimya.
Tags
beckham