MWANACHANA wa klabu ya Yanga na
mpenzi maarufu wa soka nchini, Ally Mohamed anayejulikana zaidi kwa jina
la utani ‘Ally Yanga’ amefariki dunia leo baada ya ajali ya gari
iliyotokea, eneo la Mpwapwa, Dodoma.
Taarifa zinasema Ally Yanga alikuwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge kabla ya kupata ajali hiyo barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro na kufariki hapo hapo Gari alilokuwa amepanda kuacha njia huku wengine kwenye gari hilo wakijeruhiwa.
Mwili wa Marehemu Umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam
Aliibukia Ubungo miaka ya nyuma kidogo ambako alikuwa
anafanya shughuli ya kusajili laini za simu za mkononi katika vibanda
vilivyokuwa pembeni ya kituo kikuu cha mabasi ya mikoani, Ubungo
Terminal.Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam
Na alianza kuonekana Uwanja wa Taifa pamoja na kikundi cha mashabiki wa Yanga cha Ubungo Terminal, ambako ndipo lilipokuwa tawi lake.
Ally Yanga enzi za uhai wake akiishabiki Yanga Uwanja wa Taifa katika mechi tofauti
Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.
Tags
TANZIA