BANDA MEDIA BLOG

SHERIA YA MAHOUSE GIRL BADO KITENDAWILI KIGUMU BUNGENI


MBUNGE wa Chambani,Ussi Salum Pondeza(CCM) amehoji kuhusina na Sheria ya kuwalinda wafanyakazi wa mahotelini na majumbani imekwama kutungwa Zanzibar na Tanzania Bara huku akitaka ufafanuzi Je ni sababu zipi zinazosababisha azimio kutowasiliswa bungeni.
Akiuliza swali Leo bungeni,Pondeza alidai kuwa Zanzibar haiwezi kutunga sheria zake za kulinda haki za wafanyakazi wa mahotelini na majumbani mpaka azimio hilo lipelekwe na Wizara ya Sera,Bunge,Ajira,Vijana na Walemavu bungeni na kuridhiwa.

‘’Je ni lini Bunge litapokea azimio hilo na kulinda haki za wafanyakazi hao’’aliuliza
Pia Mbunge huyo alihoji Je Serikali inavieleza nini Vyama vya Wafanyakazi wa mahotelini na majumbani ambao walianza kufanya matayarisho ya utekelezaji wa azimio hilo lakini wamekwama kutokana na mkataba huo kutoridhiwa na Bunge tangu kuafikiwa.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Anthony Mavunde alikiri kuwa mwaka 2011,Nchi wanachama wa Shirika la Kazi Duniani ILO ikiwemo Tanzania zilipitisha mkataba wa kimataifa kuhusu kazi za staha za wafanyakazi wa majumbani.


Mavunde amesema hadi sasa Nchi zilizoridhia mkataba huu ni 23 kati ya Nchi wanachama 189 ambapo kwa upande wa Afrika ni Nchi mbili tu ndio zilizoridhia ambazo ni Mkataba huo ili kufanya maandalizi ya kuridhia.
Amesema masuala ya kazi na ajira si ya Muungano ambapo alidai Tanzania Bara ina sheria zake za kazi halikadhalika Zanzibar ambazo zinawahusu wafanyakazi wote ikiwemo wafanyakazi wa mahotelini na majumbani.

‘’Kwa kuwa Nchi yetu inayosheria mbalimbali zinazotambua na kusimamia maslahi ya wafanyakazi nchini wakiwemo wafanyakazi wa majumbani na mahotelini na vyama vyao waendelee kutambua kutambua juhudi za Serikali za kulinda na kutetea haki na maslahi ya Wafanyakazi kupitia sheria kanuni na taratibu tulizonazo’’ alisema
Naibu Waziri huyo amesema Serikali itaendelea kuelimisha jamii na wadau mbalimbali kuhusu mifumo,maudhui na taratibu za uridhiaji wa mikataba ili kufanya maandalizi stahiki kabla ya uridhiaji wa mikataba hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG