BANDA MEDIA BLOG

TAARIFA KUHUSU UJIO WA RAIS WA SPECIAL OLYMPICS KANDA YA AFRIKA


Wajumbe wa Board,                                                                                               22/5/2017                                                                                                                    
Special Olympics Tanzania,
S.L.P. 42979,
DAR ES SALAAM.

                      Ndugu,

YAH: TAARIFA YA UJIO WA RAIS WA SPECIAL OLYMPICS KANDA YA AFRIKA
Rejeeni kichwa cha habari hapo juu.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwapeni  taarifa kuwa rais wa chombo chetu cha Special Olympics Kanda ya Afrika ambaye pia ni mtendaji mkuu Bw. Charles Nyambe  anatarajia kufanya ziara katika Program yetu ya Tanzania kuanzia tarehe 5/6/2017 hadi 9/5/2017.
Akiwa hapa Tanzania atapata fursa ya kuendesha mafunzo ya uongozi wa michezo ya Special Olympics  kwa makocha  50, (nimeona  wawe waratibu wetu wa mikoa yote 30, pamoja na wengine 20 kutoka Dar es Salaam).
Amependekeza  pia kutumia masaa matatu kati ya siku nne atakazokuwa nasi hapa Tanzania kukutana na kuendesha  mafunzo ya uongozi kwa  wajumbe wote wa board ya Special Olympics Tanzania.
Naomba taarifa hii itumike kama mwaliko wa kuhudhuria mafunzo tajwa hapo juu katika siku na tarehe ambayo mtatangaziwa kwa kadri atakavyopendekeza na kupanga yeye mwenyewe.
Ahsante
Charles Rays
Mkurugenzi Special Olympics Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG