Na Salim Kikeke
Mshambuliaji
wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake Jorge Mendes
kufanikisha uhamisho wake kurejea Manchester United (Sun).
Manchester United watawapa Real
Madrid David de Gea, 26, pamoja na pauni milioni 183, ili kumsajili
Cristiano Ronaldo, 32 pamoja na Alvaro Morata, 24 (Tuttosport).
Manchester United itawapa Real
Madrid David de Gea pamoja na pauni milioni 175 kumchukua Ronaldo, na
pia watamfuatilia Alvaro Morata katika mkataba mwingine tofauti (Daily
Mirror).
Iwapo De Gea atakwenda Real Madrid, Manchester United watamfuatilia kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18 (Calciomercato)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hamtaki Ronaldo kwa sababu anahisi kiwango chake kimeanza kushuka (Diario Gol).
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amempigia simu Ronaldo kujaribu kumshawishi asiondoke Madrid (Marca).
AC Milan huenda wakaamua kumfuatilia kipa wa Manchester City Joe Hart, 30, iwapo kipa wao Donnarumma ataondoka (Daily Express).
Mshambuliaji wa Manchester United
Wayne Rooney amekuwa akivutia timu mbalimbali nchini Spain, Italia,
Uturuki na Marekani pamoja na China, lakini Rooney pia huenda akaamua
kubakia Old Trafford (Times).
Chelsea wataongeza juhudi zao za
kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro, 26, pamoja na
kiungo Tiemoue Bakayoko, 22 (Guardian).
Kiungo wa Italy Marco Verratti, 24, anataka kuondoka Paris Saint Germain kwenda Barcelona (Gazzetta dello Sport).
Liverpool
bado wapo kwenye mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa winga Mohamed
Salah, 25, lakini hawataki kulipa pauni milioni 35 wanazotaka klabu hiyo
ya Seria A (Sky Sports).
Everton watafikisha pauni milioni
60 za usajili wiki hii watakapokamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa
Malaga, Sandro Ramirez, 21 (Daily Star).
Southampton wanataka kumsajili
beki wa kimataifa wa Austria, Kevin Wimmer, 24, lakini wanataka
Tottenham kupunguza bei ya pauni milioni 20 (Daily Mirror).
Leicester City wanafikiria kutoa dau la pili kumtaka beki Jonny Evans, 29 kutoka West Brom (Daily Telegraph).
Chelsea wanataka kuongeza dau kufikia pauni milioni 60 kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro (Daily Express).
Manchester United wamempa ‘ofa’ya mkataba mkubwa zaidi Blaise Matuidi, kuliko aliokuwa nao sasa PSG (PSG United).
Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 44 kumsajili winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins (A Bola).
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund
Pierre-Emerick Aubameyang huenda akaungana na meneja wake wa zamani
Jurgen Klopp, Liverpool (Le Parisien).
Barcelona watatumia kifungu cha kumnunua tena Gerard Deulefeu kwa kutoa pauni milioni 10.5 kwa Everton (Times).
Marco Asensio huenda akaomba
kuondoka Real Madrid iwapo timu hiyo itasajili wachezaji watakaomuweka
‘benchi’, huku Arsenal, Liverpool na Juventus wakiwa wamemuuliza kiungo
huyo mshambuliaji (Diario Gol).
Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 26.3 kumsajili kiungo wa Barcelona Arda Turan (AMK).
Mshambuliaji wa Arsenal Takuma Asano, 22,
atabakia kucheza kwa mkopo Stuttgart msimu ujao kwa sababu hawezi
kurejea Emirates kwa kuwa hajatimiza vigezo vya kupata kibali cha
kufanya kazi Uingereza (Daily Express).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara tu zitakapothibitishwa.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka wote. Nakutakia Jumatatu njema.
Tags
Tetesi za Usajili