
Sina kawaida ya kudharau jambo hata kama linaonekana ni la kijinga na
nimeshapata faida kubwa kutokana na mtazamo wangu huu,nimeshafanikiwa
kwenye mambo mengi ambayo watu waliyaona ni ya kijinga na wengine
walijifunza kupitia hili
Leo naomba niwashirikishe jambo hili ambalo ni mewauliza watu kadhaa na
wameonekana kunishangaa mtu kama mimi ni kwanini hasa nimeamua
kulifuatilia hili,lakini najua kupitia hili naweza kujifunza kitu ambac
ho sikua nakijua au nikajikuta napoteza muda wangu,yote haya ni matokeo
na nimejiandaa kwa yote
Kuna namba watu wamekuwa wakidai kuwa kama unataka kuzungumza na Shetani
au majini basi unaweza kuzipiga,kuna jamaa yangu aliwahi kuzipiga
nikiwa nae na simu iliita na ikapokelewa halafu aliulizwa shida yake na
alisema lakini aliepokea simu alimuambia kuwa "huwezi wewe na
usitusumbue"
Kuna jamaa yangu mwingine alipiga nae simu ilipokelewa na aliambiwa kuwa wapo busy hivyo hawahitaji usumbufu
Ukiangalia namba hizi hazina namba kiunganishi ili ujue hata location ya
namba hizi,kitu hiki kimenifanya nijiulize sana kama hii inakubalila
kwa mamlaka husika za mawasiliano
Sina ufahamu hasa wa mambo ya mawasiliano na nadhani hapa kuna watu
wengi wanaweza kunipa maelezo ya kutosha na nikaridhika kuhusiana na
dhana hii kuwa namba hizi ukipiga unazungumza na shetani au
majini,sidhani kama jambo hili halina maelezo kwa wale ambao wanajua
kuhusu mawasiliano na ndio maana nikaamua kuja kuuliza hapa ili jambo
hili niachane nalo
Namba zenyewe ni 11111111111 na 999999999 nadhani zipo na zingine,hebu wakuu nisaidieni hapo ili niweze kujua
Nikwanini hakuna namba kiunganishi lakini simu inaita?
Je ni akina nani wanaopokea simu hizi?
Karibuni ....