
Wengi walijua ni mchanga angalau sasa wanajua ni makinikia ambayo baada
ya muwekezaji kubanwa alisema ukweli yanamuingizia 50% ya kipato chake
chote, Baada ya kubanwa zaidi alisema tangu yazuiwe makontena Kila siku
anapoteza Bil 2 za kitanzania. Kabla ya hapo waliaminishwa ni michanga
isiyo na cha maana.
Wengine wakisikika kupinga kuwa michanga huwa haisafirishwi wakati miaka yote inapita hapohapo dodoma kuelekea ughaibuni ....
Angalau sasa tunaelekea kufunguliwa bongo nini ni nini katika madini
kutoka kwa Serikali, wakosoaji wake,muwekezaji,wachambuzi etc zamani
ilikuwa ni malalamiko yasiyoelekea kwenye hitimisho.
Asante JPM kwa kufukua makaburi ya akili zetu
Nguli wa madawa ya kulevya aliyetikisa dunia Pablo Escobar aliwahi
kuchoma mahakama, kukodi waasi kufanya mauaji, kufanya Kila unyama ili
sheria ya yeye au wauza madawa wenzake wasipelekwe marekani maana
kulikuwa na uwezekano 0% kutoroka au kuhonga.
Leo moja ya watuhumiwa wakubwa alihamishwa kutokea gereza la tanzania
hadi marekani kitu ambacho huwa ni pigo kubwa kwa mtuhumiwa wa drugs
popote ulimwenguni. Pablo Escobar alifananisha na kuwekwa kwenye kaburi
la CHUMA(Iron TOMB) yenye uwezekano sufuri wa kutoroka. Yale yaliyokuwa
tunadhani hayawezekani sasa yanawezekana.
Asante JPM kwa kufukua Makaburi ya Akili zetu
Ni aibu kupita sehemu kukuta kijiji kinalia njaa huku nyasi zimesitawi
mashambani bila kuwepo na zao lolote. Angalau basi pawe na mazao kidogo
yaliyokauka kama ushahidi kuwa kuna juhudi zilifanyika lakini mabadiliko
ya hali ya hewa yalikuwa kikwazo.
Hapa alionekana katili lkn ukweli ni huo uko dhahiri. Anafungua bongo
zetu kuwa kila mtu ajitume kwa kadili ya uwezo wake na akibaki
kulalamika basi atakula matunda ya malalamiko yake. Leo ni kawaida
kusikia dada mrembo young graduate akiulizia bei ya mbegu za tikiti
wakati zamani angekaa sebuleni anaangalia TV hadi muujiza wa ajira
utakapomdondokea.
Asante JPM kwa kufukua makaburi ya akili zetu.
Kuna watu walizoea kujenga majumba, kununua magari,kufanya kila aina ya
anasa kwa pesa kwa misingi ya rushwa, ujanjaujanja, udaladalali,
madilimadili, kukandamiza wasio nacho, dhuruma na uonevu. Angalau sasa
kila mmoja anaanza kufikiri upya baada ya mianya hii kuhafifishwa
kabisa.
Watu wengi wenye uwezo waliweka akili zao na uwezo wao kando na
kujielekeza kwenye njia za mikato zisizohalali ili wanufaike. Leo
angalau ni kinyume.
Kila maamuzi yana madhara yake, na wenda matatizo yanayoonekana sasa ktk
biashara baada ya muda yatapita tunaamini mambo yatakuwa sawa.
Asante JPM kwa Kufukua Makaburi ya Akili zetu
Tags
RAIS MAGUFULI