Mwalimu wa Elimu ya Mlipa Kodi
kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi
akielezea jambo wakati wa Mdahalo wa Vijana kuhusu Nguvu ya Kodi,
ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) leo
Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA Taifa Bw.
Suleiman Makwita na Muongoza mada Bi. Nuria Mshare. Kauli mbiu ya
mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya
Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akifafanua jambo
wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar
es Salaam. Kutoka kushoto ni Muongozaji wa mdahalo huo Bi. Nuria Mshare
na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi
Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya
Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Irene Kalumuna akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mdahalo hukusu kodi
ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Muongozaji wa Mdahalo wa Vijana
kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana
Tanzania (TYVA) Bi. Nuria Mshare akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo
leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA, Bw.
Suleiman Makwita na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi. Kauli mbiu ya mdahalo
huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
Washiriki wa Mdahalo wa Vijana
kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana
Tanzania (TYVA) wakichangia mada wakati wa mdahalo huo uliofanyika
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo. Mdahalo
huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Kijana katika
masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la Action Aid
Tanzania
Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa
Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya
Vijana Tanzania (TYVA) wakifuatilia mada wakati wa mdahalo huo
uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam
leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa
Kijana katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la
Action Aid.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
Tags
KODI