Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa na katika mitaa ya mji wa
Dodoma alipofanya ziara ya kushitukiza, kukagua matumizi ya mashine za
kutolea risiti kwa njia ya kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara wa
maduka mjii humo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua mashine ya EFD na risiti ya
kieletroniki aliyopewa baada ya kununua bidhaa kwenye moja ya maduka
mjini Dodoma, alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua kama
wafanyabiashara wa mji huo wanatumia ipasavyo mashine hizo.
Kiongozi wa Timu Maalumu ya
Ukaguzi wa Mashine za EFD’s kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
mkoani Dodoma, Bw. Godfrey Patrick (wa pili kushoto) akifafanua jambo
wakati wa ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), kwenye maduka mjini Dodoma.
Mfanyabiashara wa duka la rejareja
mjini Dodoma, Bw. Donald Chami, akimwonesha mashine ya kieletroniki
ambayo imeharibika, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango
(Mb), baada ya kufanyaziara ya kushitukiza kwenye duka lake na kubaini
kuwa hatoi risiti za kielektroniki kwa wateja wake.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akipitia kwa makini fomu ya makadirio ya kodi
iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika moja ya duka la
vipodozi mjini Dodoma wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya mashine
za EFD’s katika baadhi ya maduka yaliyopo mjini humo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuonya mfanyabishara wa mjini Dodoma, Bw.
Isdori Shirima, baada ya kukuta akiuza bidhaa bila kutoa risiti za
kielektroniki kwa wateja wake inavyotakiwa na kuagiza Mamlaka ya Mapato
mkoani humo kufanya ukaguzi wa kina ili kubaini kiwango cha ukwepaji
kodi cha mfanyabiashara huyo na kumchukulia hatua za kisheria.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti ya mteja aliyenunua tanki la
kuhifadhia maji katika moja ya duka linalouza vifaa vya ujenzi mjini
Dodoma, na kutoa wito kwa wananchi kukagua risiti zao ili kubaini kama
kiwango kilichoandikwa kinalingana na kiasi kilichoandikwa kwenye
risiti.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akimwelekeza mwananke mmoja aliyemkuta dukani
akague risiti yake baada ya kufanya manunuzi kwenye duka moja la vifaa
vya ujenzi mjini Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza ili kubaini
namna wafanyabiashara wa maduka mjini humo wanavyotumia mashine za
kielektroniki za kutolea risiti.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akimuagiza Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) mkoani Dodoma, Bw. Ngaka Magere, kumkutanisha na mawakala
wanaosambaza mashine za kieletroniki za kutolea risiti mkoani humo
baada ya kutoridhishwa na huduma zao
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango (Mb), akisikiliza maelezo ya matumizi ya mashine za
kielektroniki kutoka kwa mfanyakazi wa Kituo kimoja cha Mafuta mjini
Dodoma, alipofanyaziara ya kushitukiza kituoni hapo kuangalia matumizi
ya mashine hizo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akikagua risiti na kupata maelezo kutoka kwa
mhudumu wa Kituo cha Mafuta cha ORYX mjini Dodoma, Bi. Hanifa Shaldin,
alipofanya ziara ya kushitukiza kuangalia kama vituo vya mafuta mjini
humo vimefungwa mashine za kielektroniki za kutolea risiti kwa wateja
wao.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
……………………..
BENNY MWAIPAJA, DODOMA
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dokta
Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika mitaa ya mji wa
Dodoma na kubaini baadhi ya wafanyabiashara hawatumii ipasavyo mashine
za kieletroniki za kukusanyia kodi ya Serikali-EFDs na kuwaonya
wafanyabiashara kote nchini kuacha mchezo huo.
Dkt. Mpango aliyeambatana na
baadhi ya maofisa wa Mamlaka ya Mapato hapa nchini-TRA mkoa wa Dodoma
amebaini baadhi ya wafanyabiashara hao wasio waaminifu hawatoi risiti
huku wengine wakiandika kiwango kidogo cha fedha kwenye risiti hizo.
Mmoja wa wafanyabiashara
aliyekumbana na mkono wa Waziri Dokta Mpango, ni Bwana ISDORI SHIRIMA
ambaye amekiri kufanya makosa ya kutotumia mashine hizi ipasavyo
“naomba unisamehe Mheshimiwa,
sitarudia tena unajua sisi vijana tunabangaiza, lakini nimebaini
nimefanya makosa” aliomba msamaha Bw. Shirima
Hata hivyo Dkt. Mpango ameiagiza
Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA mkoa wa Dodoma, kufanya ukaguzi wa kina
wa mahesabu ya mfanyabiashara huyo ili kubaini kiwango cha kodi
alichokwepa na kumchukulia hatua stahiki.
Aidha, Dokta Mpango ameiagiza
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Dodoma kuwapeleka ofisini kwake
mawakala wote mkoani humo wanaosambaza mashine za kieletroniki za
kukusanyia mapato EFDs baada ya kubaini kuwa zaidi ya mashine 100
zimeharibika na hazitumiki tangu jana.
“Kuna kitu sikielewi na hakiingii
akilini, inakuwaje mashine ziharibike kwa kiwango hicho, mashine 100
kuharibika kwa siku mbili ni nyingi na ina maana nimekosa mapato mengi”
alielezea kwa masikitiko Dkt. Mpango.
Aliagiza mawakala wote
wanaosambaza ama kuuza mashine hizo wakutane naye ofisini kwake mjini
humo ili kubaini tatizo na kuongeza kuwa haiwezekani wafanyabishara
walipie mashine hizo zaidi ya mwezi uliopita lakini hawapelekewi hali
inayozidi kuikosesha Serikali mapato yake.
Baadhi ya wananchi na
wafanyabiashara wamepongeza uamuzi wa Serikali wa kulivalia njuga suala
la kodi na kwamba wako tayari kuiunga mkono Serikali kwa kutoa risiti
wanapouza bidhaa na kudai risiti zenye viwango sahihi vya manunuzi
waliyoyafanya ili kuijengea Serikali uwezo wa kuihudumia jamii.
Dokta Mpango ametembelea pia
baadhi ya vituo vya mafuta mjini humo na kuwakumbusha wamiliki wote wa
vituo vya mafuta kuzingatia agizo la Serikali linalowataka wafunge
mashine maalumu za kielektroniki zinazofungwa kwenye pampu za mafuta
ndani ya siku 14 ambazo ziko ukingoni.
Tags
EFDs