Prof.Mwanfupe amekuwa diwani kutokana na kuteuliwa na chama chake cha CCM kuwa diwani wa manispaa ya Dodoma.
Jumla ya kura zilizopigwa ni 58 ambapo Prof.Mwanfupe amepata kura 50 na diwani wa chadema Yona Kusaja amepata kura 8.
Akitangaza matokeo Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwini Kunambi amesema wapiga kura wote ni 58 na hakuna kura iliyoharibika na Prof.Mwanfupe ameoata kura 50 na diwani Chadema amepata kura 8.
Kunambi amemtangaza Prof.Mwanfupe kuwa Meya wa Dodoma ikiwa anachukua nafasi ya Meya wa awali Jafary Mwanyemba ambaye aliondolewa kwa nafasi hiyo kwa kupigiwa kura na madiwani wenzake kwa madai kuwa hawakuwa na imani naye.
Hisia ya kutokuwa na imani na Mwanyemba iliibuliwa na madiwani wa upinzani na kuungwa mkono na madiwani wa CCM na kupelekea kupiga kupiga kura ya kutokuwa na imani naye nakumuondoa katika nafasi yake.
Wakati huo huo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Manispaa Christina Mdeme ameapa kuhakikisha anakilinda na kukisimamia cha mapinduzi licha ya kuwa siyo mwanasiasa.
Kauli aliitoa jana alipokuwa akitoa neno la shukrani muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa madiwani.
Akizungumza mbele za madiwani Mdeme alisema kuwa yeye atahakikisha anasimamia utekelezaji wa CCM bila kuwa na hofu yoyote kwa kuwa ndiyo chama cheny serikali iliyopo madarakani.
| Diwani Yona Kusaja [CHADEMA] akizungumza jambo ukumbini hapo |
| Barozi Jobu Lusinde akipunga mkono wakati wa mkutano huo |
Naye mgombea umeya kupitia Chadema Yana Kusaja amesema licha ya kuwa kura zake hazikutosha lakini kura alizopata ni muhimu zaidi.
Amesema ili Dodoma iweze kusonga mbele ni lazima kufanya kazi kwa kutofuata mashinikizo ndani ya chana anachotoka.
Amesema prof.Mwanfupe anatakiwa kutumia elimu yake ili kuifanyamanipaa ya Dodoma kuwa na maendeleo badala ya kuwa na makundi au kujenga chuki kati ya diwani na diwani.
Naye Meya wa Manispaa ya Dodoma Prof.Mwanfupe akitoa salamu za shukrani kwa baraza la madiwani amesema yeye hawezi kufanya kazi vizuri kama hatapata ushirikiano na madiwani wenzake.
Mbali na hilo amewataka madiwani wote kuondokana na mitazamo ya itikadi na badala yake wajenge tamaduni ya kufanya kazi za maendeleo kwa faida ya Mwananchi wote.
Baada ya kumalizika kupiga kura madiwani wa chadema wamesema kuwa wamesalitiana katika kupiga kura.
Malumbano ya madiwani hao yametokana na kupigwa kura 8 kati ya 9 za madiwani wote wa Chadema.
Akizungumza nje ya ukumbi,diwani wa viti Maalum Chela Mahula amesema wanatoa siku tatu za kufanya upelelezi wa kumtambua aliye wasaliti wenzake na atakapopatikana chama kitamwajibisha.
Tags
Meya Dodoma