Kipa
Aishi Manula
yupo njia panda kujiunga na timu yake mpya ya Simba iliyoweka kambi
nchini Afrika Kusini huku akipanga kuwapigia simu viongoziwa Azam FC ili
ajue taratibu za kuingia kambini.

Manula
ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu
mpya wa Ligi Kuu Bara uliopangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 26, mwaka
huu licha ya mwenyewe kufanya siri.
Kipa huyo, anafanya siri kutokana na mkataba wake na Azam kutarajiwa kumalizika mapema mwezi Agosti, mwaka huu.
Manula alisema
kuwa yeye bado ni mchezaji halali wa Azam mwenye mkataba, hivyo ni
ngumu kwake kuihama timu hiyo kutokana na kanuni za usajili kumbana.