BANDA MEDIA BLOG

MEYA MPYA MANISPAA YA DODOMA AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI, SIASA NA WAKAZI WAKE KUTAMBUA MANISPAA HIYO SIYO SAWA NA NYINGINE NCHINI




Msitahiki Meya Prof Davis Mwamfupe akisisitiza jambo mara baada ya kuchaguliwa kwake,  kwenye Baraza maalumu la uchaguzi wa meya

Msitahiki Meya Prof Davis Mwamfupe akiteta jambo na Mbubunge wa jimbo la Dodoma Mjini Anthon Mavunde nje ya ukumbi wa Mikutano baada ya kuchaguliwa kwake jana July 19,2017


Hili Ndilo Pozi za aliyekuwa Kaimu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede Baada ya uchaguzi wa Meya mpya Pfof. Davis Mwamfupe  PICHA ZOTE NA JOHN BANDA MMILIKI WA BLOG HII

Madiwani wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa manispaa wakati Baraza Maalumu la uchaguzi wa meya likiendelea July 9,2019
Na John Banda, Dodoma
MSTAHIKI MEYA mpya wa Manispaa ya Dodoma PROF. Davis Mwamfupe  amesema imefika wakati ambao viongozi, wanasiasa na wananchi wote wanatambua kuwa manispaa hiyo haina picha ya kawaida kama ilivyo kwa manispaa nyingine hapa nchini kwakuwa macho ya ndani na nje ya nchi yanaiangalia kwakuwa ndipo makao makuu ya nchi yalipo

Akiongea katika mahijiano maalumu na kituo hiki ofisini kwake mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi hiyo na aliyekuwa kaimu Meya wa manispaa hiyo Jumanne Ngede, Mwamfupe amesema Jukumu alilonalo kwa sasa ni kuwafanya wakazi wake kutambua hilo

Aidha Meya huyo Msomi ambaye aliwahi kuwa Mshiriki wa Bunge Maalumu la Katiba na Mkufunzi wa semina mbalimbali za wabunge amesema anatambua fika kuwa Mameya wawili waliwahi kujiuzuru kutokana na ubadhilifu akiwemo aliyemtangulia Jaffary Mwanyemba kuwa tabia hiyo ni  huruka ya mtu mwenyewe hivyo linaloweka nidha katika taasisi yoyote ni ushirikishaji na ushirikishwaji katika kila jambo

Awali Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme mara baada ya uchaguzi wa meya huyo akamwambia mambo muhimu ya kuanzia kazi ikiwemo kudhibiti Ubadhirifu katika miradi ya maendeleo, kuondoa Mchwa anaevitafuna vyama vya ushirika na kahakikisha Dawa za Muhimu za  Binadamu zinapatikana katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati tena kwa bei nafuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG